SAMATTA ANAPONISHANGAZA NA REKODI YA MECHI 73 BILA GOLI






Mohamed Samatta-kiungo Mgambo JKT
Mohamed Samatta-kiungo Mgambo JKT
Na Baraka Mbolembole
Kwa mchezaji wa nafasi ya kiungo, wakati mwingine ni takwimu mbaya lakini ni kielelezo sahihi cha mchezaji mchapa kazi na mwenye ubora katika timu. Mechi 73 za ligi kuu Tanzania Bara bila kufunga goli lolote kwa mchezaji wa nafasi ya kiungo na nahodha wa timu ya JKT Mgambo, Mohamed Samatta si jambo linalomchanganya mchezaji huyo.
Samatta kaka wa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani, Mbwana Samatta tayari amecheza gemu zote 24 za klabu yake msimu huu, alicheza jumla ya mechi 25 kati ya 26 msimu wa 2013/14 ambao ulikuwa ni wa kwanza kwake katika timu hiyo ya Tanga ambayo ilimsaini akitokea African Lyon ya Temeke, Dar es Salaam.
Samatta Sr alicheza mechi 24 kati ya 26 msimu uliopita wakati Mgambo ilipopambana hadi dakika ya mwisho wasiteremke daraja.
“Sijawahi kufunga goli lolote tangu nilipojiunga na timu hii”, anasema Samatta Sr wakati nilipofanya naye mahojiano Jumanne hii. Ni wazi kwa mara nyingine Mgambo watalazimika kupambana kwa nguvu katika kila dakika iliyobaki katika gemu 6 za mwisho ili wasishuke daraja.
Ikiwa na pointi 24 katika nafasi ya 12 ya msimamo, Mgambo ipo juu kwa alama nne tu dhidi ya Coastal Union, alama 3 mbele ya African Sports (timu zote hizi za mkoani Tanga) alama 2 zaidi ya JKT Ruvu iliyo nafasi ya mwisho kwa timu zitakazoshuka, na wamelingana pointi na Kagera Sugar iliyo nafasi 11.
“Hatutashuka daraja. Tutaweka jitihada kuinusuru timu bila kujali tupo katika mazingira gani.” anasema Samatta ambaye ametoa pasi nne za magoli msimu huu.
Kumekuwa na malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wachezaji wa Mgambo kuhusiana na mishahara kuchelewa, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linachangia kushusha morali ya kawaida ya kiuchezaji kwa wachezaji.
“Kuna matatizo mengi katika timu, lakini siwezi kuyasema. Hali iko hivyo katika timu yetu. Tunakosa sapoti ya kutuongezea morali na nguvu zaidi, hasa mishahara kuchelewa. Ni uongozi tu kutowajibika kwa nafasi yao ndiko kumechangia tuwe hapa tulipo.”
Samatta Sr atamaliza mkataba wake na Mgambo mara baada ya kumalizika kwa msimu huu. ” Nitakuwa mchezaji huru mara baada ya kumalizika kwa msimu huu. Tayari nina ofa kadhaa mezani lakini kwa sasa bado mapema kuziweka wazi, sasa nahitaji kuisaidiatimu yangu ibaki katika ligi. Kubaki au kuondoka Mgambo hilo litafahamika baada ya kumalizika kwa msimu.”
Mkoa wa Tanga una timu tatu katika ligi kuu bara msimu huu lakini zote ziko hatarini kuteremka daraja. Coastal ipo mkiani kabisa mwa msimamo, Sports ikifuatia.
“Watu wa Tanga hususani wapenzi wa mpira hawapaswi kukataa tamaa wakati huu mapambano yakiendelea kwa timu zao. Waendelee kuzisapoti timu zote, wachezaji tutapambana hadi dakika ya mwisho.”
Samatta Sr anashangaza, anafundisha na rekodi yake ya mechi 73 za VPL bila kufunga goli lolote, lakini ni mchezaji gani mwingine aliyepata bahati kama yake, kucheza mfululizo katika timu ya kwanza. Kinachoshangaza ni kwamba licha ya kucheza kama kiungo, mchezaji huyo ameshindwa kufunga goli hadi sasa

Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: