WIKIENDI NI EMIRATES FA CUP TU KUANZA MABINGWA ARSENAL-HULL, IPO CHELSEA-CITY, MAN UNITED JUMATATU!


EMIRATES-FACUPWIKIENDI hii Ligi Kuu England haina Mechi na badala yake zipo Mechi za Raundi ya 5 za EMIRATES FA CUP.
FA CUP, Kombe kongwe Duniani ambalo sasa limeongezwa Jina na kuitwa EMIRATES FA CUP kutokana na udhamini wa Kampuni ya Ndege ya UAE, Emirates Airlines, itafungua dimba Jumamosi huko Uwanjani Emirates Jijini London wakati Mabingwa Watetezi Arsenal wakicheza na Timu ya Daraja la chini la Championship, Hull City.
Baadae Siku hiyo zitafuata Mechi 3 ambapo Reading watacheza na West Bromwich Albion, Watford kuivaa Leeds United na Bournemouth kucheza na Everton.
Jumapili zipo Mechi 3 ikianza ile ya Blackburn Rovers na West Ham na kufuata ile ya Tottenham na Crystal Palace.
Mechi za Jumapili zitakamilika kwa mtanange mkali huko Stamford Bridge kati ya Chelsea na Man City.
Mechi ya mwisho ya Raundi ya 5 ni Jumatatu Usiku kati ya Shrewsbury na Manchester United.
EMIRATES FA CUP
Raundi ya 5
Jumamosi Februari 20
1545 Arsenal v Hull City    
1800 Reading v West Brom          
1800 Watford v Leeds        
2015 Bournemouth v Everton       
Jumapili Februari 21
1700 Blackburn v West Ham        
1800 Tottenham v Crystal Palace
1900 Chelsea v Man City              
Jumatatu Februari 22
2245 Shrewsbury v Man United   
THE EMIRATES FA CUP 2015/16
TAREHE MUHIMU
Raundi ya 3
Ijumaa 9 Januari 2016
Raundi ya 4
Jumamosi 30 Januari 2016
Raundi ya 5
Jumamosi 20 Februari 2016
Raundi ya 6-Robo Fainali
Jumamosi 12 Machi 2016
Nusu Fainali
Jumamosi 23 Aprili 2016 & Jumapili 24 Aprili 2016
Fainali
Jumamosi 21 Mei 2016



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: