KUELEKEA JUMAMOSI-DABI: SIMBA, YANGA ZATUA KIMYA KIMYA DAR!


YANGAvSIMBAMABINGWA Watetezi wa Ligi Kuu Vodacom, Yanga wanatarajiwa kurejea Jijini Dar es Salaam hii Leo kwa Ndege ya kukodi  na kwenda mafichoni kujiandaa na mchezo wake dhidi ya mahasimu wao wa jadi Simba utakaopigwa Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Jijini Dar es Salaam, Yanga watapiga kambi yake katika Hoteli moja ya kifahari yenye hadhi ya nyota tano iliyopo katikati ya Jiji kwa ajili ya maandalizi yake ya mwisho kuelekea kwenye Dabi hiyo ya Kariakoo.
Wakati Yanga wakirejea leo Simba wenyewe wamerejea Dar jJana usiku wakitokea Mkoani Morogoro walipokuwa wameweka kambi katika Chuo cha Biblia.
Mara baada ya Timu hiyo kuwasil Kikosi kizima kilikutana na Viongozi kwa ajili ya kupewa maneno ya mwisho mwisho kuelekea kwenye pambano hilo ambapo walitakiwa kujituma na kuhakikisha wanaichapa Yanga kwenye pambano hilo.
Katika kuhakikisha wanaibuka na ushindi, tayari Viongozi wa Simba wamewataka wanachama wa Matawi yao kuhakikisha Matawi yote kila moja linachanga kiasi cha pesa Shilingi laki tano kwa ajili ya kuwapa Wachezaji kama motisha  ili waibuke na ushindi katika Dabi hii.
VPL-LIGI KUU VODACOM
Ratiba
Jumamosi Februari 20
Yanga v Simba       
Mgambo JKT v Tanzania Prisons  
Stand United v JKT Ruvu   
Mbeya City v Azam FC      
Majimaji v Mtibwa Sugar   
Toto Africans v Kagera Sugar      
Jumapili Februari 21
Ndanda FC v African Sports        
Mwadui FC v Coastal Union




Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: