WANGA AIPELEKA AZAM FC ROBO FAINALI KOMBE LA TFF


MATOKEO HATUA YA 16 BORA KOMBE LA TFF
Leo; Februari 29, 2016
Panone FC 1-2 Azam FC (Ushirika, Moshi)
Februari 28, 2016
Simba SC 5-1 Singida United (Taifa, Dar es Salaam)
Toto African 0-1 Geita Gold (Kirumba, Mwanza)) 
Februari 24, 2016
Yanga SC 2-1 JKT Mlale (Taifa, Dar es Salaam)
Februari 26, 2016
Ndanda FC 3-0 JKT Ruvu (Nangwanda, Mtwara) 
Coastal Union 1-0 Mtibwa Sugar (Mkwakwani, Tanga)
Februari 27, 2016
Mwadui FC 3-1 Rhino Rangers (Mwadui, Shinyanga) 
Prisons 2-1 Mbeya City (Sokoine, Mbeya)
Azam FC inaungana na Yanga, Simba, zote za Dar es Salaam, Ndanda FC ya Mtwara, Coastal Union ya Tanga, Geita Gold ya Geita, Mwadui FC ya Shinyanga na Prisons ya Mbeya kutinga Nane Bora ya Kombe la Azam Sports Federation 2016.
Allan Wanga shujaa wa Azam leo
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
AZAM FC imekamilisha idadi ya timu nane za kucheza Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation, kufuatia ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Panone FC jioni ya leo Uwanja wa Ushirika mjini Moshi, Kilimanjaro.
Azam FC inaungana na Yanga, Simba, zote za Dar es Salaam, Ndanda FC ya Mtwara, Coastal Union ya Tanga, Geita Gold ya Geita, Mwadui FC ya Shinyanga na Prisons ya Mbeya kutinga Nane Bora ya Kombe la Azam Sports Federation 2016.
Haikuwa kazi nyepesi kwa Azam FC kushinda mchezo wa leo, kwani walilazimika kutoka nyuma kwa bao 1-0 na kuibuka kifua mbele kwa 2-1 baada ya dakika 90 na nne za nyongeza kufidia muda uliopotezwa.
Panone walitangulia kwa bao bao la kichwa la beki wake wa kati, Godfrey Mbuda aliyemalizia mpira wa adhabu uliopigwa na beki kulia, Ayoub Masoud dakika ya 48.
Ni bao ambalo mabeki wa Azam FC hawawezi kukwepa lawama, kwani mfungaji aliruka peke yake na kumtungua kipa Aishi Manula.
Hata hivyo, beki Serge Wawa Pascal akafuta makosa ya safu ya ulinzi kwa kuisawazishia Azam FC dakika ya 64 akimalizia kwa kichwa kona ya beki wa kulia, Erasto Nyoni.
Nyoni tena akaenda kuchonga kona maridadi dakika ya 77 ambayo iliwababatiza mabeki wa Panone baada ya kutemwa na kipa wao, Mansoor Mansoor kabla ya kumkuta mshambuliaji Mkenya, Allan Watende Wanga aliyeifungia Azam FC bao la ushindi.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Said Mourad, Serge Wawa, David Mwantika, Farid Mussa, Kipre Balou, Frank Domayo/Jean Baptiste Mugiraneza dk61, Ame Ally/Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dk46, Didier Kavumbangu/Kipre Tchetche dk46 na Allan Wanga.
Panone; Mansoor Mansoor, Ayoub Masoud, Leonard Yakobo, Godfrey Mbuda, Godfrey Masubugu, Peter Mushi, Frorence Haule/Lawrence Mbawa dk80, Christopher Mshanga, Said Mohammed/Charles Steven dk83, Mohammed Habib na Said Ahmed Salum/Adam Omar dk57


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: