Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said thabit mwambungu amesema watu waache ufahari wa kuona busha ni jambo la kujivunia swala mhimu ni kwenda kufanyi upasuaji na tiba yake ni bure |
Mratibu wa Magonjwa yaliyosahaulika Tanzania Dr. Edward Kirundi kulia amesema Magonjwa ya Matende, usubi, Kichocho, Trakoma na minyoo ni magonjwa yanayosababisha Umaskini katika jamii ya Watanzania
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Magret Malenga akionekana kwa mbali meza ya kwanza akisikiliza kwa makini hotuba ya Mkuu wa Mkoa kuhusu Magonjwa yaliyo sahaulika yanayo enezwa na mbu
Zawa za kuzuia magonjwa yaliyo sahaulika ya Matende, Usubi, Kichocho, Trakoma na Minyoo
Mganga mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Songea amesema magonjwa hayo yote matano yapo la mhimu kwanza kuzingatia usafi na kumeza vidonge vitakavyo tolewa kuanzia wiki ijayo
Mwenyekiti wa Halimashauri ya Nyasa akitoa hoja kuhusu kujua kama vidonge vitakavyo tolewa kama vina madhara yoyote kwa binadamu.Alijibiwa na Mratibu wa Mafunzo hayo kuwa vidonge hivyo havina Madhara ila wanafunzi wanapo kunywa vidonge vya Minyoo lazima wawe wame shiba kwanza
Wakurugenzi wa halimashauri za Mkoa wa Ruvuma wakisikiliza semina ya kampeni ya kumeza vidonge kwa magonjwa liyo sahaulika
Viongozi mbalimbali walio hudhulia semina ya jinsi ya kutokomeza magonjwa ya Matende, Usubi, Kichocho, Trakoma na Minyoo
Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya ya Namtumbo akiwa karibu na mkurugenzi wa halimashauri ya Tunduru
Wadau kutoka maeneo mbambali ya Mkoa wa Ruvuma
Semina ya Uhamasishaji kuhusu Magonjwa yaliyosahaulika ilihusisha Wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma pamoja na waganga, waratibu na Viongozi wa kisiasa ngazi ya Halmashauri.
Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wametakiwa kumeza dawa zino zuia kuenea kwa magonjwa yaliyo sahaulika ya kiwemo magonjwa ya Matende, Usubi, Kichocho, Trakoma na Minyoo.
Mratibu wa magonjwa Yaliyosahaulika Nchini Tanzania Dr. Edward Kirundi amesema Magonjwa hayo yanatibika, cha muhimu ni kila mmoja kushiriki katika kampeni ya kya tokomeza ma gonjwa hayo kwa kutoa elimu iliyo sahihi ili kuifanya jamii kuelewa tatizo lillo mbele yao
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment