Ushahidi: Cristiano Ronaldo ndio Mwanamichezo Anayependwa kuliko wote duniani.




Inaaminika David Beckham ndio alikuwa mchezaji maarufu kuliko yoyote katika kipindi cha kuanzia 1999-2010, lakini taji hilo kwa sasa lipo chini ya mwanasoka Cristiano Ronaldo na kuna ushahidi wa kinamba kuthibitisha hilo.
 Mshambuliaji huyo wa Real Madrid amekuwa mwanamichezo wa kwanza kutimiza idadi ya mashabiki millioni 200 kwenye social media.
Ronaldo alikuwa binadamu wa kwanza kutimiza mashabiki millioni 100 kwenye mtandao wa Facebook miezi kadhaa iliyopita – na mpaka sasa anao 109.7 million followers kwenye Facebook, 49.6 million kwenye Instagram na  40.7 million katika mtandao wa Twitter.

Nahodha huyo wa Ureno ametimiza idadi ya followers million 200 wakati jumla ya followers wake walipofikia  200,058,494, kwa mujibu wa mtandao wa takwimu za social media Hookit.com.
Ronaldo anaweza kuwa nyuma ya Lionel Messi kwenye tuzo za Ballon d’Or, lakini amemuacha mbali sana mpinzani wake kwa kuwa na mashabiki wengi – ambaye hana account ya Twitter.  
Namba za Ronaldo zinamfanya aipite idadi ya jumla ya namna za mastaa wa basketball  LeBron James, Michael Jordan, Kobe Bryant, Kevin Durant na Steph Curry, ambao jumla yao wana mashabiki 187 million.
Mwaka 2015, Ronaldo alipata followera wapya  41.8 million huku robo 3 ya hao wakitokea instagram. Ana wastani wa kupata followers  135,000 kwa siku



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: