Mkuu wa wilaya ya Ulanga anayeisimamia pia wilaya mpya ya Malinyi, Christine Mndeme, amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao wanne, akiwamo Godfrey Kodi, ambaye ni mhudumu wa afya katika zahanati ya Igawa.
Mkuu huyo wa wilaya alisema awali watu wasiojulikana walivamia zahanati hiyo Februari 14, mwaka huu na kuiba mali mbalimbali zikiwemo dawa na vifaa vya umeme wa jua, hivyo uongozi wa wilaya kuamua kuifunga zahanati hiyo.
hatua hiyo iliwachukiza wananchi na kuamua kuitisha mkutano wa hadhara wa kijiji. Katika mkutano huo, wananchi hao walipiga kura za siri na nyingi kuwataja Godfrey Kodi, Rashid Kodi, Yasini Magoha na Beno Chombo, ambao ni wakazi wa kijiji hicho.
Alisema katika msako mkali ulioendeshwa kijijini hapo, mali kadhaa zikiwamo dawa na vifaa vya umeme vilivyoibwa vilikutwa vimefukiwa kwenye mfuko wa nailoni, shambani kwa mtumishi huyo.
dawa zilizokutwa shambanio humo ni pamoja na makopo matano ya dawa za kutuliza maumivu aina ya Paracetamol, makopo matatu ya Amoxilyn, Tack 77 za dawa za kuzuia kuharisha na dawa za malaria aina ya ALU zikiwemo maboksi mawili ya ALU rangi ya blue na boksi moja la ALU za rangi ya manjano, Septrin boksi moja, sola balbu moja na sola light moja.
Aidha alisema nyumbani kwa mtuhumiwa huyo baada ya kupekuliwa, zilikutwa kadi za kliniki kwa ajili ya wajawazito na watoto ambazo zimegongwa muhuri kuwa haziuzwi, ambazo zinasadikiwa alikuwa akiziuza kwa njia za magendo.
Alisema amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, Said Msomoka, kumsimamisha kazi mara moja mtuhumishi huyo wakati taratibu zaidi za kuwafikisha mahakamani zikiendelea.
CHANZO: NIPASHE
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment