Lissu alifika katika Kituo Kikuu cha Polisi, jijini Dar es Salaam saa 4.00 asubuhi jana na kuachiwa saa 7.21 mchana baada ya kukamilika kuhojiwa na kwa sasa jalada lake linashikiliwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhojiwa, Lissu bila ya kuingia kwa undani juu ya alichohojiwa, alisema aliwekwa kwa muda wa saa tatu lakini mahojiano yalifanyika kwa saa moja tu na kwamba muda mwingi ulipotea bila ya sababu.
Alisema katika hali yoyote hayuko tayari kuzibwa mdomo iwe na polisi au mahakamani, kwani haki lazima aisimamie.
UZUNGUMZIA ZANZIBAR
Lissu, alimbebesha zigo la mgogoro wa la uchaguzi mkuu wa Zanzinbar, Rais John Magufuli, akisema machafuko yakitokea moja kwa moja atahusika kama Jemedari mkuu wa nchi.
Alisema kama mgogo wa uchaguzi mkuu wa Zanzibar hautapatiwa ufumbuzi wa haraka, kuna uwezekano wa damu za wananchi kumwagika kwa machafuko.
“Awali Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alikuwa ndiye msimamizi na msuluhishi wa migogoro yote ya kisiasa Zanzibar, hivyo badala ya kusubiri Rais Magufuli kuburuzwa visiwani, atumie busara kunusuru uchaguzi huo,” alisema Lissu.
Lissu alikuwa ameongozana na mawakili wake watatu, Peter Kibatala, Hekima Muhasibu na Fredick Kilwelo.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment