Kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo tetesi za kocha Jose Mourinho kujiunga na Manchester United zinavyozidi kukua – na leo huko nchini Hispania kuna taarifa mpya juu ya makubaliano ya Jose na United.
Gazeti la kila siku la Spain ‘El Pais’ limeripoti kwamba taarifa mpya za Mourinho katika makala yake inayozungumzia matokeo mabaya ya Real Madrid.
Baada ya matokeo ya kipigo kutoka kwa Atletico juzi jumamosi, mashabii wa klabu hiyo wameanzisha mjadala wa kutaka Raisi wa klabu hiyo Florentino Perez ajiuzulu kwa sababu ameendelea kutokufanya vizuri katika kuiongoza timu hiyo hasa upande wa uajiri wa makocha wa timu hiyo.
Baada ya kumtimua Rafa Benitez wiki kadhaa zilizopita na kumteua Zinedine Zidane kuwa kocha mkuu – Madrid wameendelea kutokupata matokeo ya kuridhisha na sasa ‘El Pais’ wanaripoti kwamba baadhi ya mashabiki wanaamini Zidane hakuandaliwa vya kutosha kuwa kocha wa Real Madrid.
El Pais pia wakaendelea kusema Perez alimteua Zidane baada ya kushindwa kumrudisha Mourinho ambaye mnamo mwaka jana mwishoni Perez alikuwa na mawasiliano na wakala wa kocha huyo Jorge Mendes juu ya uwezekano wa kumrudisha The SpecialOne Santiago Bernabeu.
Lakini ghafla wakiwa hatua za mwanzo za majadiliano, Mendes akakata mawasiliano na Madrid juu ya suala la Mourinho.
Baada ya kukata mawasiliano na Madrid, Mendes akafanikisha Mourinho amefikia makubaliano ya kwanza (Pre-contract) ya kujiunga na Manchester United, na El Pais wanaripoti kwamba kwenye mkataba huo wa kwanza kuna kipengele kinachosema kutakuwa na adhabu ya fidia kubwa ikiwa aidha Mourinho au United itakwenda kinyume na makubaliano.
El Pais wanaripoti kwamba Mendes aliitumia Madrid na jaribio lao la kumtaka Mourinho ili kufanikisha dili na Manchester United.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment