Barcelona waifikia rekodi ya Real Madrid iliyodumu kwa miaka 27


Baada ya Real Madrid kupokea kipigo cha 1-0 kutoka mahasimu wao Atletico Madrid nyumbani kwao Santiago Bernabeu juzi usiku –  FC Barcelona jana waliwakaribisha Sevilla Nou Camp katika kujaribu kuongeza utofauti wa pointi dhidi ya wapinzani wao.
  Matokeo ya mchezo huo, Barcelona waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Sevilla – Magoli mawili ya Lionel Messi na Gerard Pique  yaliwezesha Barca kushinda wakitoka kuwa nyuma ya Sevilla na kufanikiwa kuweka rekodi  ya kucheza mechi 34 bila kufungwa katika msimu mmoja.  
Rekodi ya FC Barcelona ilianzia mwanzoni mwa msimu huu mara baada ya kufungwa na Sevilla mnamo October 2015, na tangu mechi hiyo Barca wamecheza mechi 34 za mashindano yote bila kupoteza na kuifikia rekodi ya Real Madrid ya msimu wa 1988-89.
Kikosi cha Real Madrid kilichokuwa chini ya kocha Leo Beenhakker na nyota mastaa kama  Butragueño, Hugo Sánchez, Michel na Schuster ndio ilikuwa timu ya mwisho Spain kuweka rekodi hiyo. Kikosi hiki cha Madrid kilifanikiwa kushinda mataji manne mfululizo ya la Liga. 
  Kikosi hicho ambacho kinatajwa kuwa moja vikosi bora kabisa vya Madrid kilianza kutengeneza rekodi hiyo mnamo September 29, 1988  na ikaenda mpaka ilipotimia michezo 34 kisha mnamo April 15, 1989, kikosi hicho kikafungwa na Celta Vigo na hivyo rekodi ya kutopoteza mechi ikaishia mchezo wa 34. 
  
Barcelona hii ya sasa inayoongozwa na MSN ya Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar, chini ya  kocha Luis Enrique imeshafanikiwa kutwaa makombe ya La Liga, Champions League na  Copa del Rey msimu uliopita na wakaja kuongeza makombe mengine mawili mwanzoni mwa msimu huu. 
  Kikosi cha Beenhakker cha Madrid kilishinda mechi 25 na kutoa sare 9, wakifunga magoli 85 na kufungwa magolu 34, wakati Barcelona wameshinda mechi 28 na sare 6, wakifunga magoli na kufungwa 19












Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: