Wananchi na wadau wa Elimu katika kata mbalimbali wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wanawalalamikia walimu wakuu wa shule za msingi kwa kuto kuwepo shuleni muda wa vipindi na kuwafundisha wanafunzi hali ambayo inaweza ikawa ni chanzo cha kupatikana kwa matokeo hasi ya kitaaluma katika shule nyingi wilayani Ludewa.
Hayo yamesemwa mapema hii leo na wananchi pamoja na wadau wa Elimu ambao wanawatoto katika shule ya Msingi Mchuchuma ambayo ipo katika kata ya Luilo na kusema kuwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi mchuchuma ni wiki tatu hadi sasa hayupo shuleni hali ambayo inaweza ikasababisha wanafunzi kufeli kutokana na kukosa kwa baadhi ya vipindi.
Aidha wananchi hao wakizungumza kwa masikitiko wamesema kuwa mwalimu huyo ndiye anaye tegemewa kuwafundisha watoto wa darasa la kwanza na darasa la pili lakini hayupo badala yake watoto hao wanafika shuleni na kucheza pasipo kupata chochote huku wazazi hao wakisema kuwa kuna watoto wanasoma darasa la tatu wa shule hiyo hawajui kuandika kabisa.
Katika hatua nyingine wazazi hao wamemtupia lawama Diwani wa kata ya Luilo Mh,Felisian Kongo kwa kuto fuatilia suala la Taaluma katika shule hiyo huku wakisema mwalimu huyo anaishi Luilo ambako ndiko yaliko makao makuu ya kata hiyo na Diwani anamwona lakini hakuna hatua stahiki ambazo anamchukulia mwalimu huyo.
Hata hivyo Redio Best fm imejitahidi kumtafuta Diwani wa kata ya Luilo na Mwalimu mkuu kwa njia ya Simu ya mkononi ili wazungumzie changamoto hiyo lakini jitihada zimegonga mwamba lakini Kituo hiki cha matangazo cha Redio Best fm kiko mbioni kuwafikia wahusika hao.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment