EUROPA LIGI: MAN UNITED HOI KWA KITIMU CHA DENMARK, SPURS SARE ITALY!



FC Midtjylland 2 Manchester United 1
MANUNITED-DENMARKFC Midtjylland, Kitimu cha Denmark kilichoanzishwa Mwaka 1999 wakati Man United chini ya Sir Alex Ferguson ndio miamba wa Ulaya walipotwaa Trebo, yaani Ubingwa wa England, FA Cup na UEFA CHAMPIONZ LIGI, chenye Uwanja MCH Arena unaochukua Watu 11,800, Leo kimeichapa Manchester United Bao 2-1 katika Mechi ya kwanza ya Raundi ya Mtoano ya UEFA EUROPA LIGI.
Man United walitangulia kufunga lakini udhaifu wa Kiungo na Difensi yao uliruhusu FC Midtjylland kupiga Bao 2 na kuwa na nafasi kadhaa za kuongeza Bao nyingine kadhaa.
Man United, wakiwakosa Wachezaji wao kadhaa kutokana na maumivu, walipata pigo kabla Mechi hii kuanza baada ya Kipa wao David de Gea kuumia Enka wakati akipasha mwili moto na nafasi yake kuchukuliwa na Kipa wa Argentina Sergio Romero.
++++++++++++++++++
MAGOLI:
FC Midtjylland 2
-Pione Sisto, Dakika ya 44
-Ebere Paul Onuachu 77
Man United 1
-Memphis Depay, Dakika ya 37
++++++++++++++++++
Timu hizi zitaruadiana huko Old Trafford Alhamisi ijayo.
VIKOSI:
FC Midtjylland: Andersen; Romer, Hansen, Bodurov, Novak; Hassan, Sparv; Kadlec, Sisto, Olsson; Pusic
Akiba: Dahlin, Urena, Dueland, Banggaard, Bach Bak, Onuachu, Royer.
Manchester United: De Gea; Love, Smalling, McNair, Blind; Herrera, Carrick; Lingard, Mata, Memphis; Martial
Akiba: Romero, Poole, Riley, Pereira, Schneiderlin, Weir, Keane.
REFA: Artur Dias (Portugal)
++++++++++++++++++
Fiorentina 1 Tottenham 1
Huko Stadio Artemio Franchi, Firenze Nchini Italy, Wenyeji Fiorentina walitoka Sare ya 1-1 na Tottenham.
Tottenham walitangulia kufunga kwa Penati ya Dakika ya 37 iliyopigwa na Nacer Chadli na Fiorentina kusawazisha kwa Bao la katika Dakika ya 59 la Bernardeschi.
VIKOSI:
ACF Fiorentina: Tatarusanu, Gonzalo, Tomovic, Astori, Alonso, Costa, Kuba, Borja, Zarate, Bernardeschi, Ilicic
Akiba: Sepe, Badelj, Vecino, Kalinic, Fernandez, Pasqual, El Babacar
Tottenham: Vorm, Trippier, Alderweireld, Wimmer, Davies, Carroll, Mason, Eriksen, Alli, Son, Chadli
Akiba: McGee, Rose, Walker, Dembele, Dier, Onomah, Kane
REFA: Felix Zwayer [Germany]
EUROPA LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 32
Ratiba/Matokeo:
Jumanne Februari 16
Fenerbahce 2 Lokomotiv Moscow 0
Alhamisi Februari 18
Sevilla 3 Molde 0
Villarreal 1 Napoli 0
Borussia Dortmund 2 Porto 0
Anderlecht 1 Olympiacos 0
Fiorentina 1 Tottenham 1
St Etienne 3 Basle 2
Midtjylland 2 Manchester United 1
[Kuanza Saa 2305]
Valencia v Rapid Vienna
Augsburg v Liverpool
Sparta Prague v Krasnodar
Galatasaray v Lazio
Sion v Braga
Shakhtar Donetsk v Schalke
Marseille v Athletic Bilbao
Sporting Lisbon v Bayer Leverkusen
**Mechi za Marudiano ni Februari 25.
KALENDA
Raundi ya Timu 32-Mechi ya Kwanza: 18 Februari
Raundi ya Timu 32-Mechi ya Pili: 25 Februari
Raundi ya Timu 16-Droo: 26 Februari, Nyon
Raundi ya Timu 16-Mechi ya Kwanza: 10 Machi
Raundi ya Timu 16-Mechi ya Pili: 17 Machi
Robo Fainali-Droo: 18 Machi, Nyon
Robo Fainali-Mechi ya Kwanza: 7 Aprili
Robo Fainali-Mechi ya Pili: 14 Aprili
Nusu Fainali-Droo: 15 Aprili
Nusu Fainali-Mechi ya Kwanza: 28 Aprili
Nusu Fainali-Mechi ya Pili: 5 Mei
Fainali: 18 Mei, St. Jakob-Park, Basel, Uswisi



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: