HII NILIWAHI KUIRUSHA SIKU ZA NYUMA.
ENZI HIZO: NYIMBO ZA YANGA NA SUNDERLAND!!!
BENDI ZILIEGEMEA KLABU: YANGA-WESTERN JAZZ, SUNDERLAND-DAR JAZZ!
KIPINDI CHA MICHEZO “MBILI KASOROBO” KILIHAMASISHA ‘NYIMBO ZA KLABU!’
KATIKA MWISHONI MWA MIAKA YA 1960, na mwanzoni mwa 1970, Klabu zetu Vigogo, Yanga na Sunderland [Sasa ndio hii Simba!], kama kawaida zilikuwa na Washabiki wake na upinzani wa Jadi ulikuwepo na Mashabiki kulumbana kulikuwepo na, tofauti na sasa, Bendi za Muziki kubwa Nchini, wakati huo, ziliegemea Klabu hizo.
Yanga na Simba, zote ni za Dar es Salaam, na enzi hizo Bendi kubwa Nchini ni pamoja na Western Jazz, iliokuwa ikiongozwa na Ahmed Kipande, na Dar Jazz, wakiwa na Mpiga Solo Nguli, Michael Enock pamoja na kina Juma Town, zote zikiwa Dar es Salaam.
Ilikuwa siri ya wazi, Western Jazz, waliokuwa Mtaa wa Sikukuu, Jirani na Makao Makuu ya Yanga wakati huo, Makutano ya Sukuma na Mafia, ni Washabiki wa Yanga, na Dar Jazz, iliochipukia Eneo la Misheni Kota, Mtaa wa Ndanda, sasa John Rupia[NILIPOZALIWA MIMI], na kuhamia, Mtaa wa Mchikichi, Jirani na Makao Makuu ya Sunderland [Hii Simba sasa] yaliyokuwepo Kona ya Mtaa wa Kongo na Mchikichi, ni Simba.
Wakati huo, ipo Redio Stesheni moja tu, Redio Tanzania [Iliitwa TBC kabla ya hapo] na kila Siku, Saa 1 Dakika 45 Usiku, maarufu Mbili Kasorobo, kulikuwa na Kipindi cha Michezo.
Mara nyingi, wakati huo, Mechi za Yanga na Simba hazitangazwi mbali ya Gossage Cup [Sasa ndio Chalenji] na yale Mashindano ya Mikoa, Taifa Cup.
Ili kupata habari za Michezo Nchini kote na Duniani, Wadau wote, daima, husikiliza Mbili Kasorobo, Kipindi cha Michezo.
Enzi hizo kulikuwa na Watangazaji wa Michezo wenye mikogo kina Salum Seif Mkamba, kina Senior Said Omari na kadhalika na wao walikuwa na ushabiki wao.
Siku Yanga na Simba wakicheza, kabla ile Nyimbo ya kuashiria Kipindi cha Michezo kuanza [Signature Tune] ukisikia moja ya Nyimbo hizi zifuatazo au Kibwagizo chake basi wewe kama Shabiki wa Timu pinzani nenda kalale mapema, maana mmefungwa!
SIKU WAKISHINDA SUNDERLAND [SIMBA]:
++NI DAR JAZZ:
YAMEWAFIKA WENZETU,
MAMBO YANAWASHANGAZA
WAMEBAKI WANALIA
TUTAFANYA JAMBO GANI
+++++++++++++++++++++++++++++
SIKU WAKISHINDA YANGA:
++NI WESTERN JAZZ:
NIPO KATI YA BAHARI
MAJI YAMENIZUNGUKA
SINA MOJA LA KUFANYA
MUNGU NISAIDIE
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment