‘DAR DERBY’ LAZIMA ROBO FAINALI FA CUP



Kazi tu

Yanga SC na Simba SC ni miongoni mwa timu 8 zitakazocheza hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho ( FA Cup). Wakati timu ya nane kufuzu kwa hatua hiyo ya nane bora ikitarajia kupatika leo Jumatatu kwa mchezo wa Panone FC v Azam FC katika uwanja wa Ushirika, mjini Moshi. Vigogo Simba na Yanga ndiyo timu pekee ambazo zilicheza na timu za madaraja ya chini.
Mwadui FC ambayo iliifunga 3-1 Rhino Rangers-timu ya ligi daraja la kwanza katika mchezo wa hatua ya 16 awali iliwashinda mahasimu wao wa mkoani Shinyanga, Stand United katika mzunguko wa tano. Wakati ni timu moja tu ya ligi daraja la kwanza ikiwa imefuzu kwa robo fainali.
Ni wazi Geita Gold Sports ilikutana na ratiba ngumu katika hatua ya 32 bora na ile ya 16 bora kwa kuwa imeweza kuzindoa timu za JKT Mgambo, kisha wameishinda Toto Africans jana Jumapili kwa goli 1-0 katika uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Tanzania Prisons iliwaondoa mahasimu wao wa Mbeya, timu ya Mbeya City FC, shukrani kwa goli la kiki ya moja kwa moja kutoka goli hadi goli iliyopigwa na mlinda lango wao Beno Kakolaki dakika ya 88,’ Prisons ni kati ya timu 6 za VPL ambazo zimefuzu kwa hatua ya robo fainali kabla ya mechi ya Jumatatu hii ya hatua ya 16 bora.
Coastal iliitoa Mtibwa Sugar timu nyingine ya ligi kuu na Ndanda SC iliwaondoa waliokuwa mabingwa watetezi JKT Ruvu. Simba iliishinda Burkina Faso (imeshuka daraja la kwanza kwenda daraja la pili) katika mchezo wa mzunguko wa timu 32.
Kisha jana Jumapili imefanikiwa kufuzu robo fainali kufuatia ushindi wa 5-1 dhidi ya Singida United (imepanda kutoka ligi daraja la pili hadi ligi daraja la kwanza.) Simba ni timu iliyotingia robo fainali baada ya kukutana na wapinzani dhaifu zaidi miongoni mwa timu zote zilizofuzu.
Yanga inafuatia kwa sababu wapinzani wao waliopita walikuwa dhaifu pia. Waliitoa Friends Rangers kisha JKT Mlale (timu zote za ligi daraja la kwanza) kama Azam FC pia watafuzu nao watakuwa miongoni mwa timu zilizopendelewa na ratiba ya hatua mbili zilizopita.
Timu hizo 3 kubwa (Yanga, Simba na Azam) sasa zinapaswa mbili kupambana zenyewe. Itashangaza Simba, Yanga na Azam kama zitapangwa na timu nyingine kila mmoja wakati awali zimepata nafuu katika mpangalio wa ratiba.
Kama ningepewa nafasi ya kupanga ratiba yangu katika robo fainali ya FA michuano ambayo itatoa mwakilishi wa Bara katika michuano ya Shirikisho Afrika hapo mwakani ningepanga hivi;
Simba SC v Yanga SC
 Mwadui FC v Panone/Azam FC
 Geita Gold Sport v Ndanda SC
Tanzania Prisons v Coastal Union



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: