CHEKA: NITAMPA KIPIGO CHA PAKA MWIZI HUYO MZUNGU, MTAONA

Cheka alisema hayo walipokutana kwa mara ya kwanza katika mkutano na waandishi wa habari iliofanyika kwenye ukumbi wa Sinema wa Mlimani City jijini.
Alisema kuwa Ajetovic amekosea kukubali kupambana na yeye katika ardhi ya Tanzania kwani mwaka 2008 alishindwa kwa pointi kutokana na maamuzi ya majaji  ambao walimpendelea.

Mabondia Francis Cheka (kushoto) na Geard Ajetovic (kulia) wakiwa wameshika pamoja mkandaa watakaogombea Jumamosi 


Promota Jay Msangi (katikati) akiutambulisha mkanda wakaogombea Cheka (kulia) na Ajetovic (kushoto) 

“Nimejiandaa vilivyo kwa ajili ya pambano hili,nilikuwa Zambia nilikfanya mazoezi ya wiki mbili, huyu jamaa ananiita mimi babu wakati wote tumezaliwa miaka ya 1980, atajuta nakuambia, amenizalilisha sana nami nitamjibu ukumbini,” alisema Cheka.
Wakati huo huo; Mkanda wa ubingwa wa mabara wa WBF utakaogombewa na mabondia Francis Cheka na Muingereza, Geard Ajetovic umewasili nchini.
Mapema rais wa WBF, Goldberg Haward na marefarii kutoka Afrika Kusini waliwasili jijini Dar es Salaam wakiwa na mkanda huo utakaogombewa na mabondia hao kesho kwenye viwanja vya Leaders.
Muda mfupi baada ya mkanda huo kutua nchini, Cheka na Ajetovic walipata fursa ya kupiga nao picha wakiwa sanjari na makocha wao, Abdallah Salehe 'Comando' na Aksu Sahhaydar.
Kwa nyakati tofauti jana, mabondia wote wawili walitambiana huku Cheka akibainisha kutotishwa na tambo za mpinzani wake huyo ambaye aliwasili nchini Jumanne iliyopita akitokea Ujerumani alikokuwa ameweka kambi.
"Siku zote naamini maneno si vitendo, sitaki kuzungumza mengi lakini nitazungumza ulingoni Jumamosi, nimesikia tambo za mpinzani wangu lakini nasisitiza tena, sijawahi kuwaangusha Watanzania nchini kwetu na sitarajii iwe hivyo Jumamosi, cha msingi ni wao kunisapotio siku hiyo," alisema Cheka.
Mkurugenzi wa Advance Security, Juma Ndambile alisema mabondia hao watapima uzito na afya Alhamis saa tano asubuhi kwenye hoteli ya Palm Beach tayari kupanda ulingoni hapo kesho.
"Kila kitu kimekamilika, kiingilio VIP itakuwa elfu 50 na viti vya kawaida ni Sh elfu 15, milango ya Leaders itakuwa wazi kuanzia saa nane mchana ambapo kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwamo ya bendi ya Twanga Pepeta kabla ya mapambano kuanza saa moja usiku yakitanguliwa na mapambano ya utangulizi.



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: