LEO Uwanjani Wembley Jijini London huko England, Manchester City wametwaaKombe la Ligi, Capital One Cup, C1C,baada ya kuibwaga Liverpool kwa Penati 3-1 baada ya Sare ya 1-1 katika Dakika 120 za Mchezo na Shujaa ni Kipa Namba Mbili Willy Caballero.
Katika Dakika 90 za kwanza, Man City walitangulia kufunga Mfungaji akiwa Luis Fernandinho katika Dakika ya 49 na Liverpool kusawazisha Dakika ya 83 kwa Bao la Phillippe Coutinho.
Kisha zikaongezwa Dakika za Nyongeza 30 na hakuna Timu iliyopata Bao na Gemu kwisha 1-1 baada ya Dakika 120 na kukaribisha Mikwaju ya Penati Tano Tano.
+++++++++++++++++++++++
Dondoo muhimu:
-Liverpool wametwaa Makombe yao yote 3 ya mwisho kwa Penati – UEFA CHAMPIONZ LIGI 2005, FA CUP 2006 na Kombe la Ligi 2012.
-Kwenye Fainali zilizoamuliwa kwa Penati Liverpool wameshinda 14 Kufungwa 3.
+++++++++++++++++++++++
Katika Mikwaju hiyo ya Penati, City walifunga Bao zao 3 kupitia Navas, Aguero na Yaya Toure huku Fernandinho akipiga Posti wakati Liverpool wakifunga Penati ya kwanza iliyopigwa na Emre Can na kukosa 3 zilizofuatia zilizopigwa na Lucas, Coutinho na Lallana ambazo zote zilichezwa na Kipa wa City Willy Caballero.
Tombola ya Penati Tano Tano:
-Liverpool=Emre Can=Goli
-Man City=Fernandinho=Anapiga Posti
Liverpool 1 Man City 0
-Liverpool=Lucas=Caballero anaokoa
-Man City=Navas=Goli
Liverpool 1 Man City 1
-Liverpool=Coutinho= Caballero anaokoa
-Man City=Aguero=Goli
Liverpool 1 Man City 2
-Liverpool=Lallana= Caballero anaokoa
-Man City=Yaya Toure=Goli
Liverpool 1 Man City 3
VIKOSI:
LIVERPOOL: Mignolet; Clyne, Lucas, Sakho, Moreno; Can, Henderson; Milner, Firmino, Coutinho, Sturridge.
Akiba: Bogdan, Toure, Benteke, Allen, Lallana, Origi, Flanagan.
MAN CITY: Caballero; Sagna, Kompany, Otamendi, Clichy; Fernando, Fernandinho; Silva, Yaya Toure, Sterling; Aguero.
Akiba: Hart, Kolarov, Zabaleta, Demichelis, Navas, Iheanacho, Bony.
REFA: Michael Oliver
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment