YANGA, MTIBWA, WAICHEKA AZAM INAYOJIANDAA KUPANDA BOAT KUREJEA DAR
Yanga wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali wakiongoza kundi lao (Kundi B) baada ya kuibuka na ushindi wa bao 2-1 katika mchezo mzuri dhidi ya Mtibwa Sugar uliochezwa January 7, 2016 usiku kwenye uwanja wa Amaan.
Mtibwa walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza lililofungwa na Kichuya lakini Yanga walisawazisha bao hilo kupitia kwa Issoufou Boubacar Garba aliyepiga mpira wa adhabu ndogo ukajaa moja kwa moja wavuni.
Yanga walipata bao lao la ushindi dakika ya 81 bao lililowekwa kambani na Malimi Busungu akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Simon Msuva.
Matokeo hayo yanaipa Yanga nafasi ya kuongoza kundi hilo baada ya kumaliza mechi zake zote ikiwa na pointi saba ikifuatiwa na Mtibwa Sugar yenye pointi nne wakati Mafunzo inakamata nafasi ya tatu ikiwa na pointi tatu huku matajiri wa jiji la Dar es Salaam Azam FC wao wameaga mashindano wakiwa na pointi mbili kufuatia kupata sare kwebye michezo miwili na kupoteza mchezo mmoja.
Yanga na Mtibwa Sugar wamefuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano ya Mapinduzi Cup mwaka 2015 na wanazisubiri timu zitakazofuzu kwenye michezo miwili itakayochezwa kesho kati ya Simba SC dhidi ya JKU wakati URA itacheza na Jamhuri.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment