LOUIS
VAN GAAL anaripotiwa kuwa karibuni kujiuzulu kuitumikia Manchester
United baada ya kukiri kwamba amewaangusha mashabiki zake.

Kocha huyo wa kidachi alizmewa sana katika dimba la Old Trafford kufuatiwa timu yake kufungwa 1-0 dhidi ya Southampton.

Mapema
jana, Van Gaal inaaminika alikuwa na mazungumzo juu ya hatma yake na
CEO Ed WOODWARD. Imeripotiwa pia wachezaji nao wamekuwa na wasiwasi juu
ya hatma ya kocha wao. Gazeti la SunSport linaripoti kwamba Van Gaal
yupo tayari kujiuzuliu kuliko kusubiri kufukuzwa. LVG alisema:
“Ninasikitika kwamba nimeshindwa kuyatimiza matarajio yao.
“Wana mategemeo au walikuwa nayo juu yangu na nimeshindwa kuyatimiza. Hivyo najisikia vibaya kwa sababu hiyo.”
Wakati huo huo jana timu ilishindwa kufanya mazoezi kama ilivyo
utaratibu wao kufanya mazoezi ya kupasha misuli siku moja baada ya
mechi.

Mjumbe
wa bodi ya United David Gill aliongeza uzito wa presha kwa Van Gaal
akisema kwamba Mdachi huyo amefanya kazi chini ya kiwango pamoja na
kupewa fedha nyingi za kuingia sokoni.
Boss huyo wa zamani wa United alisema klabu inataka timu icheze soka
la kuvutia – na Van Gaal, ambaye alisafiri kwenda Holland jana,
ameshindwa kufanikisha hilo.
Gill alisema: “Bila shaka msimu huu umekuwa sio wenye mafanikio ukiangalia na uwekezaji uliofanyika katika usajili.”
Van Gaal, 64, ametumiwa kiasi cha £250million tangu aliporithi mikoba
ya Moyes miezi 18 iliyopita lakini klabu imekuwa kifanya vibaya.
Gill aliongeza: “Siwezi kukaa hapa na kuongopa kwamba soka linavutia –
kwangu mimi, tulichokifanya zamani kilikuwa kizuri. Tunataka soka la
kuvutia.”
Ludewa yetu na maendeleo yetu
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment