Kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili barani Ulaya habari kubwa na nyingi katika mchezo wa soka ni zile zinazohusu usajili wa wachezaji kutoka timu moja kwenda nyingine.
Leo nakupa story tano ambazo zimebamba kwenye vichwa vya habari vya vyombo vingi vya habari barani Ulaya kuhusiana na tetesi za usajili wa wachezaji.
6. Liverpool kwenye mapambano na Barca kumuwania Nolito
Liverpool wameanza kumuwania Nalito na tayari wameweka kiasi cha €18 millioni kwa ajili ya kumnasa striker huyo wa Celta Vigo.
Mchezaji wa zamani wa Barcelona alikaribia kutua tena Nou Camp lakini dili hilo lilibuma dakika za mwisho kutokana na kutoafikiana kwenye offer. Arsenal pia wameonesha nia ya kumfukuzia striker huyo. (Source: talkSPORT)
5. Cahill anataka kuondoka Chelsea
Inaripotiwa beki wa kati wa Chelsea Gary Cahill amemwambia kocha mkuu wa The Blues kwamba anataka kuihama klabu hiyo kabla ya dirisha la uhamisho la mwezi January halijafungwa.
Mchezaji huyo wa England anaripotiwa kukosa nafasi mara kwa mara Stamford Bridge na hiyo ianaweza ikamsababishia kutoitwa kwenye kikosi cha England kwa ajili ya michuano ya Euro 2016 itakayofanyika Ufaransa baadaye mwaka huu. (Source: Reuters)
4. Yarmolenko amekubali kutua Arsena
Taarifa kutoka Emirates zinasema kwamba, Arsenal imekubali dau la £23 millioni kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji wa Dynamo Kiev Andy Yarmolenko.
Star huyo wa Ukraine hatosaini kujiunga na the Gunners hadi majira ya joto. Mchezaji huyo mwenye miaka 26 ameshafunga magoli 13 ndani ya mechi 22 kwenye mashindano yote akiwa kwenye kikosi cha Dynamo. (Source: Sport)
3. Arsenal imewashiwa taa ya kijani kwa Isco
Manager wa Arsenal mzee Arsene Wenger sasa anaweza kumnasa mchezaji aliyemtafuta kwa muda mrefu Isco kutoka klabu ya Real Madrd baada ya kikosi cha the Los Blancos kuwaambia walipe kiasi cha £25 millioni ili kumnasa kiungo huyo wa Hispania.
2. Chelsea kulipa £30m+Remmy ili kumnasa Vady
Chelsea imeipelekea Leicester City offer nono ya £30m pamoja na mshambuliaji Loic Remmy kwa ajili ya kuinasa saini ya Jamie Vardy mwenye magoli 16 kwenye EPL.
Claudio Ranieri bado hayuko tayari kuanza kukisambaratisha kikosi chake ambacho kinaonekana kuukimbiza ubingwa wa Premier League. (Source: Daily Mirror)
1. Lewandowski aipiga chini Premier League
Mshambuliaji wa Bayern Munich Robaert Lewandowski amevirudisha nyuma vilabu vya Arsenal, Manchester United na Man City baada ya kuweka wazi kwamba klabu pekee ambayo anataka kuitumikia ni Real Madrid endapo ataamua kuondoka Ujerumani. (Source: The Telegraph)
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment