Hatimaye usiku wa jana Lionel Andres Messi alitajwa rasmi kuwa mshindi wa tuzo ya mwanasoka bora wa dunia kwa mara 5, baada ya kuwashinda wapinzani wake Neymar na Cristiano Ronaldo.
Usiku wa jana ulikuwa na matukio kadhaa yaliyotengeneza vichwa vya habari, na mojawapo ni story ya Cristiano Ronaldo alivyoeleza ilikuwaje mpaka akaanza kuvaa jezi namba 7 na kuendelea kuitumia katika jina la brand yake ya CR7.
Mnamo mwaka 2003, akiwa kinda katika klabu ya Sporting Lisbon – Ronaldo aliwavutia wachezaji wa United katika mechi ya kirafiki na baadae wakamshawishi kocha wao Sir Alex Ferguson kumsajili.
Alipowasili Old Trafford, Ronaldo anasema alivyokutana na Sir Alex Ferguson aliomba apewe jezi namba 28, lakini Fergie akamgomea.
‘Nilipofika Man United niliomba nipewe jezi namba 28, namba ambayo nilikuwa navaa nikiwa Sporting, lakini kocha akaniambia ni lazima uvae jezi namba 7.
‘Nilikuwa naogopa kiasi kuvaa jezi namba 7 kwa sababu nilifahamu Beckham alikuwa akiivaa jezi hiyo, lakini mwishowe nikaikubali changamoto na tangu wakati huo nimekuwa jezi ambayo ni ya bahati kwangu. Kwa sababu nimeshinda kila kitu kama mchezaji nikiwa na jezi hiyo. 7 ni namba yangu ya bahati.’ – Ronaldo
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment