Ndege Wanaofanana Huruka Pamoja - Lulu




Kupitia ukurasa wake mtandaoni,staa mrembo wa Bongo Movies ‘Lulu’ amefunguka haya;

"" Kuna Msemo Unasema “NDEGE WANAOFANANA HURUKA PAMOJA” hii misemo huwa inamaana sana
Kwa akili yangu ndogo nilijaribu kuuweka huu Msemo katika Maisha ya kawaida Na nikagundua Una asilimia kubwa ya ukweli

Katika Maisha yetu ya mahusiano,urafiki,undugu,ujamaa Na hata ushabiki sio kwamba mambo yanatokeaga Kama miujiza tu,Mfano kwenye urafiki Huwezi kuwa Na Urafiki Na mtu ambaye hamuendani ki mawazo Na mtazamo,mnaweza kutofautiana Muonekano Na kila mtu nje akawa anashangaa lkn ndani yetu mna strong chemistry ambayo inawafanya muwe marafiki,kama Wewe Una character ya umbea Huwezi ukadumu Na rafiki ambaye ana character ya Ucha Mungu…itabidi upate rafiki mwenye character,maono Na mitazamo Kama yako ili kuweza kuruka pamoja
Kwenye mahusiano ya Mapenzi iko hvyo pia…mtu anaweza kuwa Na mahusiano Na mtu Na watu nje wasimuelewe imekuwaje ameamua kuwa Na mtu wa aina hyo,pengine NI mtu ambaye hawaendani kbs Kwa Muonekano wa nje…point NI ile ile kuna chemistry ambayo iko ndani Yao yenye kuwafanya wawe Na mawazo sawa,maono sawa Na tabia zinazoendana Hata Kama sio asilimia kubwa…hyo NDO inayowafanya wawe pamoja bila kujali Umri,Muonekano au kitu chochote cha Muonekano wa nje..! Iko hvyo hata Kwa watu wanaokuzunguka,wanaokupenda Na kukuchukia…utapendwa Na watu mnaoendana tu wengine ambao hamna Aina yoyote Na uendano kwanza lazima wasikuelewe Na wasikupende pia kwasababu huna ambacho wanacho moyoni Kwa kichwanihaitokei tu from no where japo Kwa akili Za kawaida unaweza ukachukulia hvyo lkn Kiukweli Hivi NI vitu ambavyo vinaanza ndani yetu(Mioyoni) Na kuonekana nje NI matokeo ya mwisho kbsa..!
Usione ajabu Wala kujisikia vibaya ukiona aina flani ya Marafiki inaondoka,Aina flani ya ndugu hupatani nao au Aina flani ya watu hawakupendi…Jua tu Hufanani Naowasikukwaze Tafuta unaofanana nao


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: