Na barnabas njenjema ,Ludewa
@best fm radio ludewa
Ludewa yetu na maendeleo yetu
Imeelezwa kuwa
kata ya Ibumi wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe ndani ya Maiaka mitano ya
Diwani wa kata hiyo kupitia CCM ni lazima wananchi wa kata hiyo wanufaike na
matumizi ya simu kwani Diwani huyo yuko mbioni kufuatilia suala la kuwepoo kwa
mawasiliano katika kata hiyo.
Hayo yamesemwa
mapema January 19 mwaka huu na Diwani wa kata ya Ibumi Mh,Edward Lezile Haule
wakati akizungumza na Redio best fm juu ya nini mipango yake ya kuanza nayo
akiwa madarakani kwa muda wa miaka mitano ya 2015 hadi 2016.
Katika hatua
nyingine Diwani huyo amesema kuwa hii leo yupo M,kani Njombe kwaajili ya
kushughulikia changamoto hiyo ya wananchi kuwa na mawasiliano kwa njia ya simu
na amewataka wananchi hao kuwa na subira katika suala hilo kwani litakamilika
kwa uwezo wa mwenyezi mungu.
Hata hivyo diwani
huyo ameongeza kuwa katika kipindi chake cha uongozi wa miaka mitano
atahakikisha changamoto ya barabara ya kutoka Ludewa ifike Ibumi inakwisha na
hakutakuwepo na mtindo wa kuogopa mvua huku akisema kwa barabara ya Ibumi
kufika katika kijiji jirani cha Kingole lazima ikamilike ndani ya miaka mitano
ya uongozi wake.
Aidha amesema
kuwa kuna changamoto ya zahanati katika kijiji cha masimavalafu lakini wananchi
walishaanza kuijenga huku akisema hilo nalo lipo kwenye mpango mkakati na
amewahakikishia wananchi wake ni lazima zahanati hiyo ianze kutumika ndani ya
miaka mitano.
@best fm radio ludewa
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment