KOMBE LA MAPINDUZI WATOTO WA MUSEVENI WAONDOKA NALO KWAO



Wachezaji wa URA FC wakishangilia ubingwa wao
Unaweza ukasema kisicho riziki hakiliki, hiyo ni baada ya timu ya Mtibwa Sugar kulikosa tena kombe la Mapinduzi Cup kwa mwaka 2016 kufuatia kupoteza mchezo wa fainali kwa magoli 3-1 dhidi ya URA ya Uganda kwenye mchezo uliochezwa usiku wa Jumatano January 14, 2016 kwenye uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.
URA walianza kupata bao la kwanza dakika ya 16 kipindi cha kwanza mfungaji akiwa ni Julius Ntambi bao ambalo lilidumu kwa dakika zote 45 za kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili Mtibwa waliongeza mashambulizi kwenye lango la URA lakini umahiri wa safu ya ulinzi ya timu hiyo ikiongezwa na nahodha wao Simeon Massa na golikpa wa timu hiyo Bwete Brian.
Peter Lwasa aliyetokea benchi ndiye aliyezima ndoto za Mtibwa kuibuka shujaa wa kombe la mapinduzi mwaka huu baada ya kutupia bao mbili kambani na kuihakikishia timu yake ushindi na kubeba ndoo ya Mapinduzi. Lwasa alipachika wavuni magoli yake dakika ya 85 na 88 kipindi cha pili.
Jafar Salum aliipatia Mtibwa bao la kufutia machozi dakika ya 90 na kuifanya timu yake imalize mchezo huo ikiwa ya pili kwa mara nyingine tena baada ya mwaka 2015 kumaliza ikiwa nyuma Simba ambao ndiyo walitwaa kombe hilo.
Mshindi wa Mapinduzi Cup ametwaa kitita cha shilingi milioni kumi taslimu wakati mshindi wa pili amejinyakulia shilingi milioni tano.
Kesho Mtibwa watarejea jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mwendelezo wa mechi za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ambapo Jumamosi watakutana na Simba SC ambao waliwatupa nje ya mashindano ya Mapinduzi kwenye hatua ya nusu fainali.


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: