Kocha mkuu wa Simba Dylan Kerr amewaangushia zigo la lawama wachezaji wake ambao ‘walizingua’ kwenye mchezo wao kwanza wa kundi A wakati wakicheza dhidi ya Jamhuri kutoka Pemba.
Kerr amesema anashangazwa na wachezaji wake kushindwa kupasia kamba wakati wanapobaki wao na golikipa kitu ambacho wamekuwa wakihifanyia kazi kila kukicha wanapokuwa kwenye mazoezi. Kerr hakusita kumtaja mshambuliaji wa kimataifa Paul Kiongera kutoka Kenya pamoja na mchezaji wa Azam Joseph Kimwaga anayecheza kwa mkopo Simba kuwa ndio wamemuangusha kwenye mchezo wa jana usiku.
“Kabla hatujafunga goli la kwanza tulipoteza nafasi nne. Joseph Kimwaga alipoteza nafasi mbili za wazi, Kiongera alikosa goli akiwa umbali wa mita tatu kutoka golini, tumemsajili mchezaji huyu kutoka Kenya ambaye anatakiwa kuwa mshambuliaji wa kiwango cha dunia lakini anashindwa kufunga goli akiwa mita tatu kutoka golini. Kimwaga ameshindwa kufunga ndani ya mita sita lakini ni vitu ambavyo tunafanya kila siku kwenye mazoezi”, alilalama kocha huyo.
“Sijali watu wanasema nini au wanafikiria nini, wachezaji wangu wengi wamecheza zaidi ya mechi 20 ukijumlisha na mechi za timu ya taifa wengine wamecheza zaidi ya mechi 29 achilia mbali mechi za kirafiki za pre season. Kwahiyo haya mashsindano tunawaachia wachezaji ambao hawajapata nafasi ya kucheza ili waoneshe uwezo wao”.
“Hii ni fursa kwao kunishawishi niwape nafasi kwenye kikosi cha kwanza wanatakiwa kuwa na njaa, lakini naona bado wanahitaji muda zaidi. Naogopa kuwatumia wachezaji wa kikosi cha kwanza kwasababu ni hatari sana wanaweza kupata majeraha ikiwa shida kwenye ligi. Kwamfano, Hassan Kessy ni majeruhi kwahiyo kumchezesha Emery ni ku-risk endapo akipata majeruhi timu itakuwa imepoteza wachezaji muhimu wa nafasi moja”.
“Kama kocha, huu ni wakati muafaka kutafuta wachezaji mbadala endapo wachezaji wengine watakosekana kwenye kikosi cha kwanza kutokana na kupewa kadi, majeruhi au wakiwa wagonjwa. Kwahiyo kwa upande wangu mashindano haya nimeamua kuwapa nafasi wachezaji ambao hawapati nafasi ya kucheza mara kwa mara”.
Licha ya kulazimishwa sare ya kufungana kwa magoli 2-2 na Jamhuri, kikosi cha Simba kilipoteza nafasi nyingi za kufunga za wazi kitu ambacho kimemkasirisha kocha wa mnyama na kuamua kuwachana live wachezaji wanaozingua.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment