Na Barnabas njenjema wa www.njenjenews.blogspot.com
Mkazi mmoja wa kijiji cha Ludewa mjini anayejulikana kwa jina la Nickolaus Haule katika kata ya Ludewa hapa mkoani Njombe anakabiliwa na kesi ya kubaka mbuzi na amepelekwa mahabusu kwa tuhuma ya kesi inayomkabili ya kumbaka mbuzi jike mweusi eneo la ipogo wilayani Ludewa.
Akisoma shtaka hilo ASP Emmanuely Mtairuka mbele ya hakimu Joakim Mwakyolo alisema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo la kumbaka mbuzi mnamo january 01 mwaka huu huko katika eneo la milima ya ipogo majira ya saa nane na dakika arobaini na tano mchana.
Aidha shtaka hilo linamkabili mkazi huyo kutokana na kifungu namba 154 [1] b na kesi yake imesomwa hii leo na itasikilizwa tena January 11 mwaka huu.
Pia kijana huyo anafanya tukio hilo la kumbaka mbuzi kwa mara ya pili sasa baada ya mwaka jana kufanya tena tukio kama hilo wilayani hapa
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment