Kocha mkuu wa kikosi cha Simba Dylan Kerr ataendelea kukumbukwa na wazanzibar wengi kutokana na kufanya kitendo cha kiungwana kwa kumsaidia mlemavu kushuhudia pambano kati ya Simba dhidi ya Mtibwa wakati wa mchezo wao wa nusu fainali ya Mapinduzi Cup.
Kerr alimchukua kijana alikua kwenye baikeli ya kiti (wheel chair) aliyekuwa amekaa sehemu ambayo asingeweza kushudia mechi hiyo kwa urahisi. Kocha huyo wa Msimbazi alikwenda na kumtoa kutoka eneo alilokuwa amekaa na kumpeleka mbele kabisa kwenye eneo ambalo lilimrahisishia kijana huyo kushuhudia mbambano bila chembe ya chenga.
Kitendo hicho kiliwafurahisha mashabiki wengi wa soka walioshuhudia kocha huyo akifanya uungwana uliotukaka na baadhi yao kumshangilia kwa kumpigia makofi.
Mechi ya Simba vs Mtibwa Sugar ilimalizika kwa Mtibwa kushinda kwa bao bao 1-0 dhidi ya Simba hivyo wakongwe hao wa soka la Tanzania kutupwa nje ya michuano hiyo lakini tukio la kocha huyo ndiyo lilikua gumzo uwanjani na lilibaki vichwani mwa mashabingi wa soka wa visiwani Zanzibar na litaendelea kukumbukwa siku zote kutokana na uungwana aliounesha mwalimu huyo wa soka kutoka England.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment