HIMID MAO, AMKA… MFUATE SAMATTA


Himid Mao
Na Simon Chimbo
Hakuna stori kubwa hivi sasa nchini katika nyanja zote za kisiasa, kijamii na kiutamaduni, zaidi ya jina la mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Ally Samatta ‘Popa’ ambaye ameteka hisia za wapenzi wa soka barani Afrika mara baada tu ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika anayecheza katika ligi za ndani (Afrika).
Kwa mchezaji aliyezaliwa na kukulia Mbagala, akacheza African Lyon, kabla ya kujiunga na Simba alipocheza kwa kipindi kisichozidi msimu mmoja, kisha kusajiliwa TP Mazembe na kuwa mchezaji bora wa Afrika wa ligi za ndani ya Afrika, hakuna maneno ya jumla ya Kiswahili ya kusifia alichokifanya Samatta.
Kaka yangu Shaffih Dauda mara kadhaa amekua akisema kuwa wakati mwingine ni vigumu kuwalaumu wachezaji wetu wa Tanzania kwa kutofika tunakopenda wafike kwa sababu ya kuwa hawana msingi mzuri ‘mfumo bora wa soka’ toka wakiwa wadogo kama ilivyo kwa mataifa ya wenzetu (Ivory Coast, Afrika Kusini, Misri n.k) ambako kuna shule nyingi za soka sanjari na vilabu mbalimbali vya soka vyenye mfumo wa kukuza vipaji kuanzia yosso (soccer academy).
Nakubaliana na hoja hiyo ya Shaffih, na ndio maana ninapata shida kutafuta maneno ya majumuisho ya alichokifanya Mbwana Samatta ambaye hajawahi pitia shule yeyote ile ya soka ama klabu iliyokua inaendeshwa kisasa kuweza kumfanya afike alipofikia.
Ukisikiliza simulizi za Mbwana wakati huo anaamka saa tisa usiku, anakimbia kutoka Mbagala hadi karume na kwingineko kufanya mazoezi, wakati mwingine akishinda njaa, inanifanya leo niamini hakuna kinachoshindikana chini ya jua, ni kujituma.
Tajiri namba moja Afrika, Aliko Dangote aliwahi kuandika katika moja ya program zake kuwa wengi tunamuona leo ni tajiri, tunafikiria alilala na kuamka tajiri. Lakini Dangote anasema imemchukua miaka 30 kufika alipo sasa.
Waswahili wanasema kuwa penye nia pana njia. Kitu kilichomsukuma Samatta aende kuomba kipande cha video ya goli lake alilowafunga Mazembe (kabla hajaenda) na kumpa wakala wake, ilikua ni chachu ya yeye kufika anakoelekea hivi sasa.
Wengine tumebaki tunarekodi picha tukiwa na wapenzi wetu, na kuzitupia mitandaoni, tumeridhika, hatuna mpango wa kutaka kwenda kuchukua nafasi zilizoachwa wazi na Samatta na Stopila Sunzu, pale Mazembe.
Wakati namuangalia kiungo mzambia Kalaba katika dimba la TP Mazembe, kuna taswira zikawa zinajengeka kichwani mwangu kuwa kama vile nilikua namuona Himid Mao Mkami aki-dictate dimba la kati la Celtic ya Uskochi ama Kaizer Chief ya Afrika kusini, hakuna kinachoshindikana chini ya jua.
Leo hii tunapomshuhudia Mrundi Saido Berahino akisumbua akili za watu Westbromwich Albion ya England ama Victor Wanyama (Mkenya) pale katika viwanja vya mtakatifu Mariamu Southampton ya England, inaniaminisha kuwa kumbe inawezekana kwa Frank Domayo ama Said Ndemla kukipiga nchini Ufaransa.
Himid Mao, tusilale mwanangu, tumfuate Samatta aliko. Hii tuzo ya Samatta ni kengele kwenu ninyi kuwa mkikaza na kutia nia, hakuna kinachoshindikana. Tuitangaze nchi yetu, tukiwa wengi nje, tutampunguzia kazi Mkwassa na wenzake kuivusha timu ya taifa


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: