FAINALI YA CAPITAL ONE CUP NI VITA YA LIVERPOOL VS MAN CITY





Kun
Goli la kichwa la Sergio Auero dhidi ya Everton kwenye dimba la Etihad limeipeleka Manchester City kwenye fainali ya michuano ya Capital One Cup.
Everton waliingia kwenye game hiyo wakiwa mbele kwa aggregate ya bao 2-1  lakini Ross Barkley aliongeza gape hilo kwa kupachika bao la mapema kwenye uwanja wa Etihad na kuipa City kazi nyingine ya ziada na kufanya Everton kuwa mbele kwa aggregate ya mabao 3-1 mbele ya Man City.
Kun 1
Fernandinho alisawazisha bao hilo na kuirejesha timu yake mchezoni baada ya shuti lake kumgonga beki wa Everton na kujaa kambani.
Kevin De Bruyne aliyeingia akitokea benchi alikunganisha krosi ya Raheem Sterling na kuiweka mbele Man City kwa bao 2-1 lakini aggregate ikisoma 3-3.
Kun 2
Aguero alipachika wavuni bao lililoipa ushindi City kutokana na pasi nzuri kutoka kwa De Bruyne.
Kiungo huyo wa Ubeligiji baadaye alitolewa nje ya uwanja kwa machela baada ya kuangua vibaya wakati anawania mpira na Ramiro Funes Mori.
Kun 4
City watacheza na Liverpool mchezo wa fainali ya kombe la Capital One February 28 mwaka huu kwenye uwanja wa Wembley.
Kila mmoja aliyeangalia marudio ya goli la pili tulilofungwa inaonekana dhahiri mpira ulikuwa umetoka nje ya uwanja. Mchezo ul;ikuwa mzuri sana lakini hatukutarajia kufungwa goli katika mazingira kama yale. Ni ngumu sana kulikubali hilo.
Kun 3
Kauli ya kocha wa Everton Roberto Martinez: “Kila mmoja aliyeangalia marudio ya goli la pili tulilofungwa inaonekana dhahiri mpira ulikuwa umetoka nje ya uwanja. Mchezo ul;ikuwa mzuri sana lakini hatukutarajia kufungwa goli katika mazingira kama yale. Ni ngumu sana kulikubali hilo”.
“City ni timu nzuri. Kama wangefunga magoli matatu kwa njia sahihi nasi unakubali. Goli la kwanza mpira ulimgonga mtu lakini lile la pili mpira ulikuwa nje kabisa ya uwanja”.
“Tuna wachezaji wengi viajana wazuri. Naamini tunachukulia mchezo huu kama hamasa kwetu”.
Kauli ya kocha wa Man City Manuel Pellegrini: “Nafurahi kucheza kucheza fainali Wembley, ni muhimu sana. Tulistahili kucheza fainali, tulifungwa kwenye mchezo mmoja tu dhidi ya Everton lakini tulinyimwa penati ya wazi”.
“Walitufunga 1-0 na ilikuwa ni goli la faulo ya wazi. Kama unafikiri kwasababu ya ule mpira wa Sterling hiyo siyo sababu pekee iliyotufanya sisi tushinde”.
“Tumeshindwa kwasababu tumefunga magoli matatu na Everton wamefunga goli moja”.



udewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: