Said Karsandas Pandram, Tanga
Kutokana na matoke omabayo yanayoikumba klabu ya Coastal Union ya Tanga, wanachama wa klabu hiyo wameutaka uongozi wa timu hiyo kujiuzulu kwa kuwa wameshindwa kuiendesha timu.
Wanachama hao wakizungumza kwa jazba wamesema matatizo yanayoikumba timu hiyo ni mengi kama wachezaji kucheeleweshewa mishahara pamoja na kambi duni.
Abdul Famau yeye amesema matatizo yote yanayoikumba klabu yao yamesababishwa na mkurugenzi wa hadhi na sheria wa TFF Eliud Peter Mvela kwani ndiye aliyeuvuruga uchaguzi mkuu wa klabu yao kwa maslai ya kikundi cha watu.
Kwa ujumla kwa umoja wao wameutaka uongoiz wa timu hiyo kukaa pembeni.
Oscar Assenga msemaji wa timu hiyo yeye kwa upande wake amesema matokeo mabovu yanawaumiza hata wao viongozi hivyo amewaomba wanachama wa timu hiyo kushikamana ili kuinusuru timu yao.
Pia Assenga amekataa kuweka wazi mikataba ya udhamini kutoka kampuni ya Pembe pamoja na TSN kwa madai kuwa hawezi kufanya hivyo mpaka viongozi wa juu wa kalbu watakapokutana kwani kunaweza kuwa na vitu ambavyo havipo sawa.
Wasikilize hapa wadau wakitoa maoni yao walipopiga story na Said Karsandas jijini Tanga.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment