Michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) inatarajiwa kufanyika Julai – Agosti mwaka huu kisiwani Zanzibar, taarifa ya Baraza la Vyama vya Soka kwa ukanda huo imesema.
Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye amesema pamoja na michuano ya vilabu kufanyika visiwani Zanzibar mwaka huu, pia wamejipanga kuendesha michuano ya U17 itakayofanyika Mei nchini Uganda, michuano ya Mpira wa miguu wa Wanawake (Uganda), Mashindano ya vijana chini ya miaka 20 (Burundi) huku michuano ya CECAFA Senior Challenge ikipangwa kufanyika nchini Sudan.
Mwishoni mwa wiki uongozi wa Kamati ya Utendaji wa CECAFA ulikutana nchini Sudan na kufanya kikao chake cha kwanza chini ya Rais Dkt Mutasim Ghafar amabye pia ni Rais wa Chama cha Soka nchini Sudani (SFA).
Katika kikao hicho, CECAFA ilitangaza kumpa Leodgar Tenga Rais wa heshima wa Cecafa huku pia wakisaini makubaliano ya uendelezaji wa soka la vijana na Chama cha Soka cha Saudi Arabia (SAFF) kupitia kwa Rais wake Ahmed Alharbi.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment