Mtoto Aman Vishwakarma akipatiwa matibabu.
Uttar Pradesh, India
MTOTO wa miaka 10, Aman Vishwakarma amenusurika kifo baada ya kuanguka kutoka ghorofa ya nne hadi chini kisha kuchomwa na nondo huko Uttar Pradesh nchini India.
Madaktari wakionesha kipande cha nondo walichokitoa kwenye mwili wa Aman Vishwakarma.
Inasemekana kuwa, Aman alipatwa na mkasa huo alipokuwa juu ya paa la ghorofa hiyo (ambapo ni nyumbani kwao) akifanya usafi ndipo akadondoka na kuchomwa na nondo yenye urefu wa futi nne, iliyozama kuanzia kwenye mgongo na ikatokeza kwenye makalio huku nondo hiyo ikikosa kidogo tu kuchoma kwenye uti wa mgongo wa mtoto huyo.
Nondo ilivyozama kwenye mwili wa Aman Vishwakarma.
Aman anayetokea katika Wilaya ya Kaushambi mjini Uttar Pradesh nchini humo, amepona baada ya kufanyiwa upasuaji kwa saa nne na madaktari bingwa wa hospitali ya Narayan Swaroop waliofanya kila juhudi za kukitoa kipande hicho cha nondo na kufanikisha kuokoa maisha ya mtoto huyo.
Mama wa mtoto huyo, Kamla Devi (30) alizirai baada ya kuona hali ya mwanaye hospitalini hapo.
Picha ya X-Ray.
Madaktari wamesema, ilikuwa kazi ngumu kwa kuwa nondo hiyo ilichana mshipa wake mkuu wa damu, kudhuru uti wa mgongo na mapafu pia hivyo kusababisha lita 2 za damu kuvujia kwenye tumbo la chakula.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
About Rafiki Fm Ludewa
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment