Waziri Nape Akanusha Wizara Yake Kukataza Wanawake Kuvaa Mavazi ya Kubana


Waziri wa Habari, Utamaduni Wasanii na Michezo Nape Nnauye, amekanusha taarifa iliyosambaa mitandaoni inayohusu wizara yake kukataza baadhi ya mavazi hasa sehemu za mikusanyiko ya umma.

Amesema Taarifa hizo ni za uzushi na uongo, na kuwataka mamlaka husika kuwachukulia hatua watu waliotoa taarifa za uongo.

“Hizo taarifa ni uzushi mtupu na uongo, mamlaka husika wachukue hatua, watimize wajibu wao, watumie sheria iliyopo kuwachukulia hatua”, amesema Mh. Nape Nnauye.

Mwishoni mwa wiki hii kuna taarifa ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha ni taarifa kwa vyombo habari juu ya katazo la mavazi yasiyofaa kwenye mikusanyiko ya watu, hususan hospitali, maofisini, sokoni, na vyuoni.



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: