Mkuu wa wilaya ya ludewa Anathori Choya amewataka wazazi wote wilayani ludewa kuweza kuwaandikisha watoto wote wanao takiwa kuanza darasa la kwanza kwa mwaka 2016 ili waweze kupata elimu bora kwa wakati muafaka hasa kwa kipindi hiki ambapo ambapo serikali imefuta gharama za ulipaji wa michango mashuleni.
Akizungumza na njenje habari blog ofisini kwake amesema kuwa wazazi wote wenye watoto wanao takiwa kuanza darasa la kwanza Wakawaandikishe mashuleni kwao na kuwa hato sita kuwachukulia hatua za kisheria wale watakao wakalisha watoto hao nyumbani kwani wengi wao walishindwa kutokana na gharama za uandikishaji
Aidha choya ameongeza na kuendelea kuwakumbusha wananchi wa wilaya ya ludewa kuendeleza suala la usafi ambao unategemea kufanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi na kuwaomba kuonyesha ushirkiano ili kuweza kuweka mazingira safi na kuepukana na magonjwa ya mlipuko wilayani hapa.
Hata hivyo CHOYA amesema kuwa jukumu la kufanya usafi ni jukumu la wananchi wote hivyo kuwaomba mabwana afya kuweza kusimamia kiukamilifu zoezi hilo ili kuweza kutekeleza na kutii agizo la MH,John pombe Magufuli la kufanya usafi mara moja kwa mwezi.Pamoja na hayo amesema kuwa hato sita kuwachukulia hatua za kisheria wale ambao watakiuka maagizo hayo ikiwa ni pamoja kuanza na viongozi wasimamizi ili kuweza kuboresha wilaya hii na kuwa mfano kwa wilaya nyingine zote...
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment