Wakazi wa kata ya Mpanga Kipengele Wilaya ya Mbarali Mkoani mbeya, wamelalamikia shirika la Hifadhi ya Taifa Mpanga Kipengele, kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji na kupora ardhi yao.
Mlalamiko hayo yametolewa katika mkutano wa hadhara uliohUsisha wananchi, uongozi wa Halmashauri ya Mji Rujewa na uongozi wa Hifadhi hiyo, mkutano ambao umelenga kumaliza mgogoro uliopo.
Katika mkutano huo, wananchi wakiongozwa na diwani wa kata hiyo Peter Vicent wamesema, wameshtushwa na kuona mpaka unazidi kusogea katika maeneo yao pasipo kushirikishwa na vitendo vya unyanyasaji na kipigo kutoka kwa wafanyakazi wa hifadhi hiyo.
Aidha wananchi hao wameomba meneja wa pori hilo kuihamisha kambi ya watumishi wake kutoka makazi ya watu na kwenda hifadhi ya ombi ambalo limekubaliwa.
Hifadhi hiyo yenye ukubwa wa skwea mita za mraba 1,574 ilitangazwa oktoba 10,2012 kwa hifadhi ya akiba ya Mpanga Kipengele ambayo mipaka yake imekuwa ikihamishwa mara tatu na kuleta sintofahamu kwa wananchi wanaozunguka eneo hilo
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment