VPL-KUREJEA WIKIENDI NI KITIMTIM AZAM FC-SIMBA, YANGA MKWAKWANI, JUMAPILI DABI YA TANGA


LIGI KUU VODACOM
RATIBA
Jumamosi Desemba 12
Kagera Sugar v Ndanda FC
Stand United v Mwadui FC
Mbeya City v Mtibwa Sugar
Azam FC v Simba
Majimaji v Toto Africans
Mgambo JKT v Yanga
Jumapili Desemba 13
JKT Ruvu v Tanzania Prisons
Coastal Union v African Sports
+++++++++++++++++++++++++++
VPL-SIT-LOGOBAADA ya Vakesheni ya Wiki kadhaa, Ligi Kuu Vodacom, VPL, Wikiendi hii inarejea kwa kishindo kwa mitanange mikali ikiwepo ile Mechi ya mvuto mkubwa kati ya Vinara wa Ligi Azam FC na Simba huku Mabingwa Watetezi Yanga wakiwa Mkwakwani, Tanga kucheza na Mgambo JKT wakati Jumapili Uwanjani hapo hapo ipo Dabi ya Tanga kati ya Coastal Union na African Sports.
Baada ya Mechi 9 Azam FC wapo juu kwenye VPL wakiwa na Pointi 25 wakifuatiwa na Mabingwa VPL-DES11-STANDWatetezi Yanga wenye Pointi 23 kisha Mtibwa Sugar Pointi 22 na Simba wapo Nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 21.
Kwenye Mechi za Wikiendi hii, huenda baadhi ya Timu zikawa zina Wachezaji wapya baada ya kuimarisha Vikosi vyao kwa kutumia Dirisho la Uhamisho la Kipindi hiki.
Simba wao wamemrejesha Straika kutoka Kenya, Paul Kiongera, na pia kuwanunua Beki wa African Sports, Novat Makunga, na Straika wa Mtibwa Sugar Haji Ugando.
Azam FC wao wamemchukua Kipa Ivo Mapunda ambae alizidakia Klabu kubwa hapa Nchini nan je ya Nchi alipokuwa na Gor Mahia ya Kenya na Saint George ya Ethiopia.
LIGI KUU VODACOM
Mechi zijazo
Jumatano Desemba 16
African Sports v Yanga
Jumamosi Desemba 19
Yanga v Stand United
Mwadui FC v Ndanda FC
Kagera Sugar v African Sports
Tanzania Prisons v Mtibwa Sugar
Toto Africans v Simba
Majimaji v Azam FC
Jumapili Desemba 20
JKT Ruvu v Coastal Union
Mbeya City v Mgambo JKT
Jumatano Desemba 23
Azam FC v Mtibwa Sugar
Jumamosi Desemba 26
Ndanda FC v JKT Ruvu
Yanga v Mbeya City






Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: