ROONEY ATAKIWA CHINA KWA GHARAMA KUBWA HAIJAWAHI KUTOKEA


MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amepewa ya Pauni Milioni 75 kwenda kuungana na kocha Sven Goran Eriksson nchini China.
Ligi Kuu ya China inamtaka mshambuliaji huyo wa Manchester United akawe nyota wao mpya, na ipo tayari kumpa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 Mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Pauni Milioni 25 kwa msimu.
Hivyo kituo kipya cha kazi cha Rooney akiamua kuondoka Old Trafford — kinaweza kuwa Shanghai SIPG, ambayo iko chini ya kocha wa zamani wa England, Eriksson.

Wayne Rooney anatarajiwa kulipwa Pauni Milioni 25 kwa mwaka ili aondoke Manchester United kuhamia Ligi Kuu ya China

Kititia cha malipo kitahusisha haki ya matumizi ya picha ambayo itamuwezesha Rooney kupata fedha nyingi zaidi iwapo ataisaidia kukua kwa umaarufu wa CSL (Ligi Kuu ya China).
CSL, ambayo pia inamtaka Nahodha wa Chelsea, John Terry, inataka Rooney ambaye amebakiza Mkataba wa miaka mitatu Man United, ajiunge nao haraka iwezekanavyo.


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: