Waziri wa Kilimo Uvuvi na Mifugo Bw Mwigulu Nchemba akisalimiana na mbunge Mteule wa jimbo la Ludewa Bw Deo Ngalawa.
....,,.........................,....,..,......,..,,,
Na NJENJE HABARI BLOG ,LUDEWA
MBUNGE Mteule wa jimbo la Ludewa mkoani mkoani Njombe Deo Ngalawa atoa salama za Krismasi na Mwaka Mpya kwa wananchi wa Ludewa na kuwataka kufanya kazi ili kwenda na kauli mbiu ya Rais Dr John Magufuli ya Hapa Kazi Tu .
Akitoa Salam zake za Krismasi na Mwaka Mpya jana aliwapongeza wananchi wake kwa kumaliza uchaguzi salama na kusherekea sikukuu ya Krismasi kwa utulivu na kuwaomba wanapoingia katika kuaga mwaka pia kujitathimini kwa kila mmoja juu ya nini alifanya kwa mwaka 2015 na kuwa na Malengo makubwa kwa mwaka 2016.
(Bw Ngalawa ambae anasubiri kuapishwa ili kuanza safari yake ya kuwatumikia wana Ludewa kwa kipindi cha miaka mitano baada ya kumbwaga mgombea wa Chadena wa Demokrasia na maendeleo ( Chadema )Bw Bartholomew Mkinga katika uchaguzi mdogo .
Alisema kuwa ni matumaini yake wananchi wake baada ya uchaguzi sasa ni wakati wa kufanya Kazi kwa bidii .
Bw Ngalawa aliwataka wananchi wa Ludewa kuendelea kuwa wamoja ili kuifanya Ludewa kusonga mbele na kuwa makundi ya uchaguzi huo kwa sasa yavunjwe kwa wote kufanya Kazi ya kujiletea maendeleo na yeye Kama mbunge wao atafanya Kazi na ccm , Ukawa na wasio na vyama .
Kwa mujibu wa Matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi jimbo la Ludewa Bw Wiliam Waziri alisema kuwa Jumla ya wananchi 65,238 walijiandikisga kupiga kura katika uchaguzi huo uliofanyika jumapili
Ila kati ya hao wananchi
31,994 walishiriki kupiga kura na kura 177 kati ya hizo ndizo ziliharibika na
Kura Halali ni 31,812 wakati Mgombea wa
CCM alipata kura 23,861
Sawa na asilimia 74.9 na Mgombea wa Chadema akipata kura 7,956
Sawa na asilimia 25.1 na kwa Matokeo hayo CCM ndio washindi katika uchaguzi huo
" kwa mamlaka niliyopewa na tume ya Taifa ya uchaguzi naomba kumtangaza Bw Deo Ngalawa kuwa mbunge wa jimbo la Ludewa na kumkabithi hati yake ya ubunge"
MWISHO
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment