NAPOLI DHIDI YA AS ROMA NI ZAIDI YA GEMU.


napoli vs romaNi wikend nyingine tena ambapo Ligi Kuu ya soka nchini Italia maarufu kama Serie A itaendelea tena kwa siku za kesho,jumapili na siku ya jumatatu.
Macho ya wapenzi wa Serie A yatakuwa katika uwanja Estadio San Paolo ambapo Napoli watakuwa wenyeji wa AS Roma.
Napoli kwa sasa inashika nafasi ya tatu baada ya kukubali kichapo toka kwa Bologna cha magoli 3-2 juma lililopita katika uwanja wa Renato D’alla.
Ushindi wao wa jana dhidi ya timu ya Legia Warszawa wa magoli 5-2 unaweza kurudisha molari ya wachezaji kuweza kukabiliana vyema na AS Roma jumapili.
Fomu ya Napoli ni nzuri sana ndani ya Serie A na nje ya serie A katika michuano ya Ulaya.Swali ni kuwa Napoli wanaweza kuhimili presha ya AS Roma?
Hakuna shaka kuwa AS Roma kwa sasa hawafanyi vzirui kwani mara ya mwisho kwa timu hiyo kushinda mchezo ilikuwa ni mwezi 11 walipowafunga wapinzani wao wa mji wa Roma timu ya Lazio kwa magoli 2-0.
Baada ya hapo AS Roma hawajashinda tena mpka hii leo.Hali hii imeonekana kuwachukiza sana mashabiki wa Roma kwani hivi karibuni walionesha chuki zao kwa kupanga matenga ya karoti barabarani ili kuzuia msafara wa klabu ya AS roma uliokuwa unatoka mazoezi.
Tamko la hivi karibuni la Rais wa klabu ya Roma James Pallota la kuwataka mashabiki wa AS Roma kuwa na moyo wa subira na timu hiyo inapitia kipindi cha mpito inaweza kuwafanya mashabiki wa timu hiyo kurudisha imani kwa timu yao na kuendelea kuipa nguvu ya ushangiliaji katika michezo ya Serie A.
Klabu za AS Roma na Fiorentina zinaonekana kuwa na safu nzuri ya ushambuliaji kwani mpaka sasa wmefunga magoli 30 katika Serie A huku Napoli wakiwa wamefunga magoli 28 tu.
Lakini safu ya Ulinzi ya Napoli inaonekana imara zaidi ya Roma kwa kuruhusu magoli 12 tu huku Roma wakiwa wameruhusu magoli 18 mpaka sasa.
Ubovu wa AS Roma katika safu ya ushambuliaji unatokana na kutokuwepo kwa ‘Chemistry ‘bora pamoja na kutokuwa na uzoefu wa kimashindano kwa wachezaji wake Lucas Digne,Kostas Manolas,Antonio Rudiger na Alexandre Florenzi.
Hakuna shaka idara ya kiungo ya AS Roma inafanya vizuri kwa uwepo wa Radja Nanggolan,Milarem Pjanic na Danielle De Rossi.
Nachokiona ambacho kocha wa Roma Rudi Garcia anapaswa kukifanya ni kumrudisha nyuma kiungo wake mkabaji Danielle De Rossi ili acheze na Kostas Manolas kama mabeki wa kati .
Halafu katika nafasi ya kiungo wa kukaba Nainggolan acheze sambasamba na Keita wakati timu ikimsubiri kiungo wake mahiri Kevin Strotman apone majeraha aliyonayo.
Mpaka sasa kuna mgawanyo mzuri sana magoli katika idara zote za klabu ya Roma kwani mpaka sasa kiungo mshambuliaji Milarem Pjanic anaongoza kwa ufungaji akiwa na magoli 7 ya Serie A.Wachezaji wengine kama Mohamed Salah ana magoli 5, Gervinho ana magoli 6.
Napoli wana rekodi nzuri sana msimu huu dhidi ya vigogo wa Serie A.Kwani tayari wameshazifunga timu za Juventus,Lazio,Fiorentina na Inter Milan.
Napoli wanajivunia sana safu yake ya ushambuliaji ikiongozwa na mfungaji bora wa Serie A mpaka sasa Gonzalo Higuian mwenye magoli 14.
Lakini ukiacha Higuain,pia nyota wengine kama Lorenzo Insigne,Jose Maria Callejon na Marek Hamsik wamekuwa msaada mkubwa sana katika safu ya ushambuliaji.
Kuondoka kwa kiungo Gokhan Inler kulionekana kuwapa mashaka mashabiki wa Napoli lakini usajili wa kiungo wa Brazil Allan toka Udinese umeonakana kuziba pengo la Inler na amekuwa msaada mkubwa sana kwa safu ya kiungoakishirikiana na Jorginho.
Huwezi kutaja uzuri wa klabu ya Napoli pasipo kuitaja safu ya ulinzi ya klabu hiyo inayoongozwa na kipa wa zamani wa klabu ya Liverpool Pepe Reina.
Pepe Reina kwa kushirikiana na na nyota wengine wa idara ya ushambuliaji kama Elseid Hysaj,Faouz Ghaloum,Raul Albiol na Kalidou Koulibaly wanafanya vizuri sana katika idara ya ulinzi.
Msimu uliopita,Napoli walipata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya AS Roma katika uwanja wa San Paolo.


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: