MINGANGE: BOBAN NI MTU POA SANA, WATU HAWAJUI TU KUISHI NAYE


Boban
Boban
Kocha mkuu wa Mbeya City Meja mstaafu Abdul Mingange amesema kuwa anavutiwa na kiwango kinachooneshwa na wachezaji wake Ramadhani Chombo ‘Redondo’ pamoja na Haruna Moshi ‘Boban’ tangu wamejiunga na timu hiyo.
Mingange amesema watu wanashindwa kumwelewa kwa kuamua kuwasajili wachezaji hao lakini yeye amesema wachezaji hao bado wanauwezo wa juu na wanawasaidia wachezaji wake wengine vijana kupata uzoefu wa ligi.
Haruna Moshi 'Boban' (kushoto) na Ramadhani Chombo 'Redondo'
Haruna Moshi ‘Boban’ (kushoto) na Ramadhani Chombo ‘Redondo’
Kuhusu Boban kuhuishwa na matukio ya ‘kitukutu’ kocha huyo amesema Boban ni mtu poa sana hasa pale unapojua namna ya kuisi nae. Pia kocha huyo wa zamani wa Ndanda FC ametoboa siri ya jinsi ya kuishi na Boban na kuongeza kuwa kama ukimzingua nyota huyo wa zamani wa Simba na timu ya Taifa lazima akuzingue pia.
Redondo
Redondo
“Boban na Redondo bado ni wachezaji wazuri sana kwasababu wote wanauwezo mkubwa na uzoefu wa juu wa soka la Tanzania. Mbali na wao kuwa na uwezo mkubwa lakini wanawasaidia vijana wetu kupata uzoefu ambao bado ni wageni kwenye ligi”, alisema Mingange jana kabla ya kuanza kwa mchezo wao dhidi ya Yanga.
“Watu hawajui tu kuishi na Boban lakini kama kocha lazima ujue kuishi na wachezaji wa kila aina. Boban hapendi kupelekeshwa, ni mchezaji ambaye anajituma kwenye mazoezi na muda mwingine anafanya mazoezi yake binafsi kwa ajili ya kujiweka fiti zaidi”.
“Sasa akiwa anafanya mazoei yake wewe ukaenda kumkatisha na kutaka kumpa programu nyingine mnaweza kupishana, sasa mimi huwa namwacha na ndio maana tunaishi vizuri”.
Kocha mkuu wa Mbeya City Meja mstaafu Abdul Mingange
Kocha mkuu wa Mbeya City Meja mstaafu Abdul Mingange
“Mimi najua kukaa na wachezaji kwasababu nimefundisha kuanzia ngazi ya vijana wakati huo nikiwa shule ya Makongo na hiyo imenisaidia kujua namna ya kuishi na mchezaji wa aina yeyote ile, lakini Boban ni miongoni mwa wachezaji wangu wazuri na hatukumsajili kwa kubahatisha



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: