Mashabiki wa klabu ya soka ya Leicester City ya nchini England jana usiku walikunywa beer za bure kama shukrani kutoka kwa wamiliki ya namna walivyoshiriki katika kuisapoti timu yao hadi sasa ligi ikiwa katikati wanashika nafasi ya pili.
Beer hizo ziligawiwa kwa kila shabiki kabla ya mechi yao dhidi ya Manchester City iliyomalizika kwa sare tasa ya bila kufungana, huku maji yakigawiwa kwa watoto na vijana waliochini ya miaka 18.
Makamu mwenyekiti wa timu hiyo aliandika kupitia program notes kuwa, “kumekua na matukio mbalimbali 2015, vita yetu ya kukwepa kushuka daraja msimu uliopita, mwanzo mzuri msimu huu, rekodi mbalimbali zimewekwa na klabu, haijawahi kutokea katika historia ya klabu hii.”
“Tunawashukuru sana mashabiki wetu kwa sapoti ya timu yao, mwaka 2015 ni wa kukumbuka milele, na sasa tunaingia 2016 katika hali nzuri zaidi tofauti na msimu uliopita ambapo tulikua tunahangaika mkiani mwa msimamo wa ligi” ameandika kiongozi huyo.
Leicester wako katika nafasi ya pili nyuma ya Arsenal huku wakiwa wamepoteza michezo miwili tu, dhidi ya Arsenal na dhidi ya Liverpool msimu huu ikiwa ndio kwanza katikati. Wamefanikiwa kutoa sare na Manchester City katika mchezo huo wa jana usiku, na sasa kila mtu anasubiri kuona kama itakuaje hadi mwisho wa msimu.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment