Stephen Curry hakuanza vyema mchezo wa alfajiri ya Jumanne. Alikosa mitupo yake kadhaa, baadhi ikiwa dhidi ya mdogo wake wa damu, Seth Curry ambaye anachezea klabu ya Sacramento Kings. Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa wao kukabiliana katika mchezo rasmi wa NBA.
Stephen Curry alimaliza mchezo na pointi 23 akatoa pasi 10 huku akidaka rebound nyingi zaidi katika maisha yake ya NBA, 14. Klay Thompson alimaliza mchezo na pointi 29, Draymond Green yeye akafunga pointi 25. Warriors sasa wameshinda michezo 33 mfululizo ya nyumbani.
Omri Caspi alifunga pointi zake nyingi zaidi katika maisha yake ya NBA, 36 kwa upande wa Sacramento Kings. Mdogo wa Stephen Curry, Seth Curry alimaliza mchezo akiwa na pointi 7. Alipata mtupo mmoja kati ya 6, huku akipata mitupo yote huru, 5.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment