MAJI PUANI: VAN GAAL-"NAWEZA KUAMUA KUNG'OKA MWENYEWE"



MANUNITED-LVG-KILIOBOSI wa Manchester United Louis van Gaal amesema anaweza kuamua kwa hiari yake kuachia ngazi baada ya Jana kupokea kipigo cha 4 mfululizo huko Britannia Stadium walipochapwa 2-0 na Stoke City.
Huku kukiwa na uvumi mkubwa kwa Mdachi huyo ambae Kikosi chake hakijashinda katika Mechi 7 kuwa atafukuzwa, Jana akihojiwa na Wanahabari baada ya Mechi hiyo ambayo walishushwa hadi Nafasi ya 6 kwenye Ligi Kuu England, aliulizwa ikiwa anahofia kufukuzwa.
Van Gaal alijibu: "Hilo ni jambo nitajadiliana na Ed Woodward (Mtendaji Mkuu wa Man United) na si wewe!"
Van Gaal aliongeza: "Si lazima Siku zote Klabu ikufukuze. Wakati mwingine unaweza kuamua mwenyewe. Lakini mimi nataka kwanza kuongea na Bodi ya Man United, Wafanyakazi na Wachezaji lakini si nyinyi!"
Mechi inayofuata kwa Man United ni Uwanjani Old Trafford Jumatatu Usiku dhidi ya Mabingwa Watetezi Chelsea ambao nao Msimu huu wako taabani kiasi cha Wiki iliyopita kumfukuza Meneja wao Jose Mourinho na kumteua Guus Hiddink kama Meneja wa muda hadi mwishoni mwa Msimu.
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
**Saa za Bongo
Jumatatu Desemba 28
1800 Crystal Palace v Swansea             
1800 Everton v Stoke                 
1800 Norwich v Aston Villa         
1800 Watford v Tottenham         
1800 West Brom v Newcastle               
2030 Arsenal v Bournemouth                
2030 Man United v Chelsea                  
2030 West Ham v Southampton            
Jumanne Desemba 29
2245 Leicester v Man City 
Jumatano Desemba 30
2245 Sunderland v Liverpool                
Jumamosi Januari 2
1545 West Ham v Liverpool                  
1800 Arsenal v Newcastle           
1800 Leicester v Bournemouth              
1800 Man United v Swansea                 
1800 Norwich v Southampton               
1800 Sunderland v Aston Villa              
1800 West Brom v Stoke            
2030 Watford v Man City            
Jumapili Januari 3
1630 Crystal Palace v Chelsea               
1900 Everton v Tottenham

@soka in tanzania

Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: