Kichwa cha nguruwe chakutwa kwenye sinki la choo wanachotumia Waislamu


Kichwa cha nguruwe kimekutwa kwenye sinki la choo wanachotumia kutawadhia wanafunzi Waislamu wa Chuo Kikuu cha Australia Magharibi kilichiko kwenye mji wa Perth Nchini Australia.

Tukio hilo limebainika ikiwa imepita witi tangu vichwa 14 cya nguruwe vilipotupwa kwenye kituo cha kuhifadhia wakimbizi nchini uholanzi.

Kichwa hicho kimegunduliwa na mwanafunzi kutoka Tunisia katika chuo hicho wakati alipokuwa akijitayarisha kusali katika msikiti uliopoo eneo la chuo.

”Hisia ya kwanza niliyopata ilikuwa ni kuona nimelengwa kutishwa.Sikutarajia kitu kama kile alisema mwanafunzi huyo aliyetambulika kwa jina la Majdi Faleh.

Aliongeza kusema kuwa hiyo si kwa sababu ya kuwa ni kichwa cha nguruwe,bali hata kama kingekuwa kitu kingine au kichwa cha mnyama mwingine,lakini ujumbe uliokusudiwa ulikuwa wa wazi kabisa kwamba hatakiwa kuwapo hapo.Polisi katika mji huo wa Perth wameanzisha uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: