Halima Mdee achangisha mamilioni kwa ajili ya kujenga Daraja

MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), amefanya harambee kwa wananchi wa Kata ya Bunju ‘A’ jijini Dar es Salaam ili kupata fedha za kujenga daraja.

Akizungumza mwishoni mwa wiki katika mkutano na wananchi, Mdee alisema fedha hizo zitatumika kujenga daraja katika kata hiyo ili kutatua kero ya usafiri kwa wananchi hao hasa kipindi cha mvua.

Mbali na harambee hiyo, Mdee aliwaahidi kuwapatia wakazi hao Sh milioni 5 kutoka mfuko wa jimbo ili kukamilisha ujenzi huo.

“Hii barabara ni kwa ajili ya matumizi ya jamii nzima hivyo ni jukumu letu sote kuchangia, naamini mtaniunga mkono kabla ya sikukuu ya Krismasi kalavati ziwe zimeshawekwa, lakini ili tufanikishe jambo hilo ninawaomba wananchi mtoe fedha hizo mlizoahidi,” alisema Mdee.

Wakizungumzia kero zao kwa mbunge huyo, baadhi ya wananchi wa eneo hilo walisema mbali na kero ya miundombinu ya barabara wanakabiliwa na ukosefu wa maji safi na salama pamoja na shule.

Maua Shaweji, mkazi wa Gurumawe alisema wapo watu wenye uwezo wa kuunganishiwa maji hadi kwenye makazi yao lakini wanawanyanyasa kwa kuwauzia ndoo moja au mbili tu za maji.

“Mimi ninaishi hapa tangu mwaka 1974, tumenyanyasika sana na maji tulidhani kwa kuwa watu wenye uwezo wamefika mtaani kwetu tungepata ahueni ya tatizo la maji badala yake ni tatizo zaidi kwani ukienda kuomba maji unapewa ndoo mbili tu ambazo huwezi kuzitumia ukiwa na familia,” alisema Maua.




Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: