Aliyemchinja mama yake kisa ni hiki



IMG_0818
Kijana Erasto Kilaini anayedaiwa kumuua mama yake.
Na Waandishi Wetu, UWAZI
DAR ES SALAAM: Simulizi inauma! Baada ya Erasto Kilaini, 23, (pichani) mkazi wa Mtaa wa Fida Hussein, Vingunguti Kiembembuzi, Dar kumchinja mpaka kumuua mama yake mzazi, Margaret Kilaini (47) na jirani yao, Mama Alonso, chanzo cha unyama huo kimejulikana, Uwazi lina kisa kamili.
Erasto ambaye pia ni marehemu, anadaiwa kutenda ukatili huo, Desemba 18, mwaka huu nyumbani kwao huko, hali iliyoacha simanzi mpaka sasa.
IMG_1651
Marehemu Margaret Kilaini enzi za uhai wake.
WALIVYOSEMA WANAOJUA
Kwa mujibu wa mtu mmoja aliyesema ni rafiki wa mtuhumiwa, chanzo cha Erasto kufanya tukio hilo ni kukosea masharti ya mganga wa kienyeji, jambo lililomfanya achanganyikiwe na kuwa mnyama kiasi hicho.
Mtu huyo (jina lipo), alisema siku ya tukio, Erasto na vijana wenzake watatu ambao hakuwataja majina, walikwenda kwa mganga huyo kwa lengo la kutaka dawa ya utajiri baada ya kuchoshwa na ugumu wa maisha.
WAPEWA SHARTI LA KUCHINJA PAKA
“Mganga aliwapa masharti kuwa kabla ya kuwapa dawa ya utajiri wa ghafla, wakachinje paka na kumfukia.
IMG_0930TUKIO LA AJABU
“Walitoka kurudi maskani huku wakiwa tayari kutimiza sharti hilo. Mara, alipita paka, Erasto akaokota jiwe na kumpiga, paka akashindwa kukimbia. Erasto alimshika na kumchinja. Cha kushangaza, baada ya kumchinja na kumfukia kama mganga
livyosema, paka zaidi ya ishirini walitokea ghafla huku wakilia milio ya ajabu. Mzee mmoja aliyekuwa akipita aliwaambia kwamba kwa walichokifanya (kumchinja paka), watarajie jambo kubwa kutokea mtaani.
IMG_0924
Mwili ukiagwa kwa ajili ya mazishi.
“Erasto na wenzake wakakimbilia kwa yule mganga na kumweleza kilichotokea. Mganga akawaambia wamekosea, waliyemchinja hakuwa paka bali mtu (mchawi) na wale paka wengine ni wachawi wenzake.
“Aliwataka watoe fedha zaidi ili awafanyie zindiko wasiguswe na wachawi hao kwa kuwa wamejitangazia vita, lakini wao walipuuza, wakaondoka wakiamini kuwa, mganga huyo anawatapeli.”
IMG_0929
….Wakiendelea kuaga.
“Siku hiyohiyo usiku, Erasto aliporudi nyumbani, alimkuta mama yake akizungumza na mama Alonso lakini kumbe alikuwa akimshitakia kutokana na tuhuma za Erasto kumchoma bisibisi mtoto wa mama Alonso. Erasto alipomwona mama Alonso, aliamini alikwenda kumshitaki kwa mama yake.
“Akamwambia Mama Alonso wewe mwanamke nilikuwa nakutafuta sana. Akachukua panga na kuanza kumcharanga kisha akamalizia na kumchinja nalo.
Mama yake alipoingilia kati, alimgeuzia kibao, akamchinja na kufa palepale huku akimkatakata vipande. Mimi naamini hayo yote yalitokana na athari ya nguvu za giza za wale paka,” kilisema chanzo.
IMG_0938JIRANI AFUNGUKA
Jirani aliyeshuhudia mauaji hayo kupitia dirishani, Allan Mwaisemba, alisema mtaa huo mara kwa mara umekuwa na mauzauza ambapo kuna kipindi watu 12 waliuawa mfululizo mpaka ikafika mahali baadhi ya watu waliamua kuhama.
“Mimi siamini hayo mambo lakini kwa mtaa wetu huu naamini. Mwaka 2006, watu 12 walikufa kiajabu akiwemo baba yake Erasto. Tena alifia mikononi mwangu. Naumia sana kuona familia yake inateketea hivi. Mimi ningekuwa mzima ningemzuia Erasto asifanye unyama ule kwa kuwa nilikuwa namwona na nilipiga kelele kumzuia,” alisema Mwaisemba ambaye ana majeraha miguuni baada ya kupata ajali ya gari.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wakati wa kuaga miili, waombolezaji walikuwa wakiupita wa Erasto bila kutoa machozi wala kuonesha hali ya huzuni lakini waombolezaji hao walipofika kwenye jeneza la mama yake vilio vilitawala.
IMG_0944WAAGWA KANISANI
Ibada ya mwisho ya kuiombea miili ya Margaret na Erasto ilifanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Vingunguti na kupumzishwa katika nyumba ya milele kwenye Makaburi ya Pugu Sekondari jijini Dar.
Imeandaliwa na Chande Abdallah, Deogratius Mongela, Boniphace Ngumije na Mayasa Mariwata




Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: