WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO LUDEWA KUBADILI NAMBA ZA VYOMBO



Meneja wa TRA katika wilaya ya Ludewa hapa mkoani Njombe amewataka wamiliki wa vyombo vya moto kama vile pikipiki pamoja na Bajaji kuendelea na mchakato wa kubadiliT namba za vyombo hivyo kutoka T hadi MC.

Akizungumza na Redio best fm mapema hii leo meneja huyo anayejulikana kwa jina la Zabroni Walwa amesema kuwa mchakato wa kubadili namba za vyombo hivyo kutoka herufi T kuelekea MC unaendelea kwani mwisho wa zoezi hilo ni mwezi December 31 mwaka huu.

Bw,Zabroni ameongeza kwa kuwataka wananchi waondokane na dhana ya kuogopa kufikisha vyombo hivyo vya usafiri katika cha polisi cha Ludewa kwani kuna mkaguzi mkuu wa vyombo hivyo ambaye anakagua na kutoa taarifa za chombo hicho ili taarifa hizo mmiliki wa pikipiki azipeleke katika ofisi za TRA wilaya ya Ludewa tayari kwa kubadili platenamba ya chombo husika.

Katika hatua nyingine meneja huyo ametoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya moto kama  pikipiki na bajaji kutii sheria bila shuruti kwani ikifika December 31 mwaka huu ni mwisho wa zoezi hilo na baada ya hapo hatua kali za kisheria zitachukua mkondo wake huku akisema watumiaji wa vyombo hivyo watambue kuwa motorvehicle imefutwa ila imebaki FIRE.


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: