**Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku, isipokuwa inapotajwa
Jumanne Novemba 3
KUNDI A
Real Madrid 1 Paris St Germain 0
Shakhtar Donetsk 4 Malmö FF 0
KUNDI B
Man United 1 CSKA 0
PSV 2 VfL Wolfsburg 0
KUNDI C
FC Astana 0 Atletico Madrid 0
Benfica 2 Galatasaray 1
KUNDI D
Borussia Mönchengladbach 1 Juventus 1
Sevilla 1 Man City 3
Real Madrid na Manchester City zimefuzu kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, baada ya Jana kushinda Mechi zao za Nne za Makundi yao na kubakisha Mechi 2.
Wakicheza kwao Santiago Bernabeu Jijini Madrid na kutawaliwa hasa Kipindi cha Kwanza, Real Madrid walipata Bao lao pekee na la ushindi katika Dakika ya 35 na kuichapa Paris St Germain 1-0 katika Mechi ya Kundi A la UCL.
Ushindi huo wa Real na ushindi wa Shakhtar Donetsk, katika Mechi nyingine ya Kundi A, ambao waliwatwanga Malmo 4-0 huko Ukraine hapo Jana, umewasaidia Real kusonga Raundi ya Mtoano.
Licha ya kufungwa, PSG wanaweza kuungana na Real kufuzu ikiwa watashinda moja ya Mechi zao 2 zilizobaki.
Toka Kundi D, Man City pia imeweza kufuzu kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Timu 16 baada ya Jana kuibamiza Sevilla Bao 3-1 huko Spain na pia kusaidiwa na Sare katika Mechi nyingine ya Kundi hili ambapo Borussia Moenchengladbach na Juventus walitoka 1-1 huko Germany.
City wamefuzu kuingia Mtoano wakiwa na Mechi 2 mkononi huku katika Mechi nyingine ya Kundi D,
Katika Mechi ya City na Sevilla, Raheem Sterling aliwapa City Bao la Kwanza katika Dakika ya 8 na Fernandinho kupiga Bao la Pili Dakika 3 baadae.
Sevilla walifufuka na kupata Bao 1 kupitia Mfaransa Benoit Tremoulinas kwenye Dakika ya 36 lakini Bao la Dakika ya 81 la Wilfried Bony liliwaua Sevilla 3-1.
Huko Germany, Fabian Johnson alitangulia kuipa Borussia Moenchengladbach Bao katika Dakika ya 18 lakini Stephan Lichtsteiner aliisawazishia Juve kwenye Dakika ya 44.
Juve walibaki Mtu 10 kwa Dakika 35 za mwisho baada ya Hernanes kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku, isipokuwa inapotajwa
Jumatano Novemba 4
KUNDI E
Barcelona v BATE Borislov
Roma v Bayer Leverkusen
KUNDI F
Bayern Munich v Arsenal
Olympiakos v Dinamo Zagreb
KUNDI G
Chelsea v Dynamo Kiev
Maccabi Tel Aviv v FC Porto
KUNDI H
KAA Gent v Valencia
Lyon v Zenit Saint Petersburg
Jumanne Novemba 24
KUNDI E
2000 BATE Borislov v Bayer Leverkusen
Barcelona v AS Roma
KUNDI F
Arsenal v Dinamo Zagreb
Bayern Munich v Olympiakos
KUNDI G
FC Porto v Dynamo Kiev
Maccabi Tel Aviv v Chelsea
KUNDI H
2000 Zenit Saint Petersburg v Valencia
Lyon v KAA Gent
Jumatano Novemba 25
KUNDI A
Malmö FF v Paris St Germaine
Shakhtar Donetsk v Real Madrid
KUNDI B
2000 CSKA v VfL Wolfsburg
Man United v PSV
KUNDI C
1800 FC Astana v Benfica
Atletico Madrid v Galatasaray
KUNDI D
Borussia Mönchengladbach v Sevilla
Juventus v Man City
Jumanne Desemba 8
KUNDI A
Paris St Germain v Shakhtar Donetsk
Real Madrid v Malmö FF
KUNDI B
PSV v CSKA
VfL Wolfsburg v Man United
KUNDI C
Benfica v Atletico Madrid
Galatasaray v FC Astana
KUNDI D
Man City v Borussia Mönchengladbach
Sevilla v Juventus
Jumatano Desemba 9
KUNDI E
Bayer Leverkusen v Barcelona
Roma v BATE Borislov
KUNDI F
Dinamo Zagreb v Bayern Munich
Olympiakos v Arsenal
KUNDI G
Chelsea v FC Porto
Dynamo Kiev v Maccabi Tel Aviv
KUNDI H
KAA Gent v Zenit Saint Petersburg
Valencia v Lyon
TAREHE MUHIMU:
-Ratiba Mechi za Makundi:
Mechidei 1: 15/16 Septemba
Mechidei 2: 29/30 Septemba
Mechidei 3: 20/21 Oktoba
Mechidei 4: 3/4 Novemba
Mechidei 5: 24/25 Novemba
Mechidei 6: 8/9 Decemba
Raundi za Mtoano:
-Droo ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16: Desemba 14
**Mechi Februari 16/17/23/24 na Marudiano Machi 8/9/15/16
-Droo ya Robo Fainali: Machi 18
**Mechi Aprili 5/6 na Marudiano Aprili 12/13
-Droo ya Nusu Fainali: Aprili 15
**Mechi Aprili 26/27 na Marudiano Mei 3/4
FAINALI
Mei 28
San Siro, Milan, Italy
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment