UEFA CHAMPIONZ LIGI
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku, isipokuwa inapotajwa
Jumanne Novemba 3
KUNDI A
Real Madrid 1 Paris St Germain 0
Shakhtar Donetsk 4 Malmö FF 0
KUNDI B
Man United 1 CSKA 0
PSV 2 VfL Wolfsburg 0
KUNDI C
FC Astana 0 Atletico Madrid 0
Benfica 2 Galatasaray 1
KUNDI D
Borussia Mönchengladbach 1 Juventus 1
Sevilla 1 Man City 3
NDANI ya Old Trafford hapo Jana Manchester United wamemaliza ukame wa Mabao kwa kuifunga CSKA Moscow Bao 1-0 kwa Bao la Kichwa la Kepteni wao Wayne Rooney katika Mechi ya Marudiano ya Kundi B la UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL.
Kabla ya Mechi hii, Man United walikuwa na ubutu wa Magoli kwani walikuwa hawajafunga Bao lolote katika Dakika 90 tangu Anthony Martial aliposawazisha walipotoka 1-1 na CSKA Moscow Wiki 2 zilizopita na tangu hapo, Man United imeambua Sare za 0-0 mara 3, mbili zikiwa za Ligi Kuu England dhidi ya Man City na Crystal Palace na moja na Middlesbrough katika Capital One Cup ambalo walitolewa kwa Penati 3-1.
Hizo zilikuwa ni Jumla ya Dakika 325 za Michezo bila kuona nyavu.
Lakini katika Dakika ya 79 ya Mechi ya Jana, ikiwa ni Dakika ya 404 tangu wafunge Bao, Michael Carrick alitoa pande murua kwa Jesse Lingard ambae Krosi yake iliunganishwa kwa Kichwa cha nguvu cha Wayne Rooney kilichomshinda Kipa Akinfeev na kuipa Man United Bao.
Hilo ni Bao la 237 la Rooney kwa Man United na kumfanya awe sawa na Dennis Law wakiwa ni wa Pili katika Ufungaji Bora katika Historia ya Man United ambayo anaongoza Sir Bobby Charlton akiwa na Mabao 249.
Ushindi huu wa Man United umewapa Man United uongozi wa Kundi B wakiwa na Pointi 7 baada ya Mechi nyingine ya Kundi B kumalizika PSV 2 Wolfsburg 0.
Mechi inayofuata kwa Man United ni hapo Novemba 25 Uwanjani Old Trafford dhidi ya PSV Eindhoven.
VIKOSI:
Manchester United: De Gea; Young, Smalling, Blind, Rojo; Schweinsteiger, Carrick; Lingard, Mata, Martial; Rooney
Akiba: Romero, Jones, Darmian, Pereira, Herrera, Depay, Fellaini.
CSKA Moscow: Akinfeev; Fernandes, Ignashevich, Berezutski, Schennikov; Dzagoev, Wernbloom; Tošić, Natcho, Milanov; Musa
Akiba: Chepchugov, Vasin, Nababkin, Golovin, Panchenko, Doumbia
REFA: Szymon Marciniak (Poland)
UEFA CHAMPIONZ LIGI
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku, isipokuwa inapotajwa
Jumatano Novemba 4
KUNDI E
Barcelona v BATE Borislov
Roma v Bayer Leverkusen
KUNDI F
Bayern Munich v Arsenal
Olympiakos v Dinamo Zagreb
KUNDI G
Chelsea v Dynamo Kiev
Maccabi Tel Aviv v FC Porto
KUNDI H
KAA Gent v Valencia
Lyon v Zenit Saint Petersburg
Jumanne Novemba 24
KUNDI E
2000 BATE Borislov v Bayer Leverkusen
Barcelona v AS Roma
KUNDI F
Arsenal v Dinamo Zagreb
Bayern Munich v Olympiakos
KUNDI G
FC Porto v Dynamo Kiev
Maccabi Tel Aviv v Chelsea
KUNDI H
2000 Zenit Saint Petersburg v Valencia
Lyon v KAA Gent
Jumatano Novemba 25
KUNDI A
Malmö FF v Paris St Germaine
Shakhtar Donetsk v Real Madrid
KUNDI B
2000 CSKA v VfL Wolfsburg
Man United v PSV
KUNDI C
1800 FC Astana v Benfica
Atletico Madrid v Galatasaray
KUNDI D
Borussia Mönchengladbach v Sevilla
Juventus v Man City
Jumanne Desemba 8
KUNDI A
Paris St Germain v Shakhtar Donetsk
Real Madrid v Malmö FF
KUNDI B
PSV v CSKA
VfL Wolfsburg v Man United
KUNDI C
Benfica v Atletico Madrid
Galatasaray v FC Astana
KUNDI D
Man City v Borussia Mönchengladbach
Sevilla v Juventus
Jumatano Desemba 9
KUNDI E
Bayer Leverkusen v Barcelona
Roma v BATE Borislov
KUNDI F
Dinamo Zagreb v Bayern Munich
Olympiakos v Arsenal
KUNDI G
Chelsea v FC Porto
Dynamo Kiev v Maccabi Tel Aviv
KUNDI H
KAA Gent v Zenit Saint Petersburg
Valencia v Lyon
++++++++++++++++++++++++++++
TAREHE MUHIMU:
-Ratiba Mechi za Makundi:
Mechidei 1: 15/16 Septemba
Mechidei 2: 29/30 Septemba
Mechidei 3: 20/21 Oktoba
Mechidei 4: 3/4 Novemba
Mechidei 5: 24/25 Novemba
Mechidei 6: 8/9 Decemba
Raundi za Mtoano:
-Droo ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16: Desemba 14
**Mechi Februari 16/17/23/24 na Marudiano Machi 8/9/15/16
-Droo ya Robo Fainali: Machi 18
**Mechi Aprili 5/6 na Marudiano Aprili 12/13
-Droo ya Nusu Fainali: Aprili 15
**Mechi Aprili 26/27 na Marudiano Mei 3/4
FAINALI
Mei 28
San Siro, Milan, Italy
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment