SECONDARY SCHOOL sehemu ya 24




















SECONDARY SCHOOL

Sehemu Ya 24

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

Ilipoishia Jana →↓↓

"mungu wangu... hebu subiri kwanza usiondoke...... zaiiii...zaaiiiii....weeeeee zaiiiiii?"
"abeee dada?"
"njooo haraka..... na wewe unakubali tu kirahisi rahisi si ndio? sasa leo mtanikoma na huyo mwenzio"
"weeee zai wee?"
"nakuja dada"
Zai alipokuja dada nusura akamswalika bonge la swali...
"zai? kabla sijakushushia kibano naomba uniambie yule mtoto wa kiume pale unamchukuliaje yule?"
"dada? yule si mdogo wangu yule?"
"Aaahaa ni mdogo wako sio?"
"ndiooo"
"ulimpa nini rafiki yako ili atembee na sheby?"

TELEZA NAYO



Yaani huezi amini dada zai anaweza kuniuza mimi daahh. Kiukweli hata mimi roho iliniuma sana baada ya kuona kwamba huyu dada kunifata haikua hiari yake, bali alipewa pesa na zai. kwani huyu dada inaonekana kwao sio watu wa hali ya kipesa hivyo ndio maana zai akamtumia huyu dada kutokana na umbo na sura yake jinsi ilivyo nzuri. Kiukweli nilimshukuru sana dada nusura kwa kuingia, maana hii ni laana ambayo kwa upande wangu siihitaji itokee.
"zai? kabla sijakushushia kibano naomba uniambie yule mtoto wa kiume pale unamchukuliaje yule?"
"dada? yule si mdogo wangu yule?"
"Aaahaa ni mdogo wako sio?"
"ndiooo"
"ulimpa nini rafiki yako ili atembee na sheby?"
"lakini si laki mbili tu dada?"
"kwaio wewe unamuuza mdogo wako wewe kwanini lakini? yaani badala wewe ndio upewe pesa kwa ajili yake, Eti wewe ndio unato pesa kwa ajili yake.. ivi ni akili yako kweli?"
"dadaa?? lakini si unaona hali ya mdogo wety haituridhishi humu ndani na hata mama haipendi, coz inapaswa tujivunie tuna ndugu wa kume ila sii wa kiume"
"zai? zai? zai? chunga domo lako ilo ntakuzaba mibao sasa hivi"
Zai aliondoka kwa hasira huku akitupa tupa mikono kwa dharau
"haya na wewe tokaaaa mfate kinyago mwenzio uko"
Alimfukuza na yule nusura mwenzie huku akinifata mimi na kunishika kichwa
"sheby?? najua haitoishia hapa, kwani hata mama mwenyewe anapenda akuone ukiwa na mwanamke ili tu roho yake iridhike"
"kwaio sasa we unanishauri vp kama dada angu?"
"ushauri wangu mimi nataka siku moja uwaonyeshe kama na wewe unaweza, mimi nakujua mdogo wangu hivyo sina wasi wasi na wewe kabisa"
"ok poa nitafikiria hilo swala"
"shika hii pesa"
"ya nini sasa hio?"
"sio ndio ulikua umetongozewa nayo hii"
"aaaa kampe mwenyewe aliompa"
Dada nusura alikua ananipa ile laki mbili ambayo alimpokonya nusura huyu dada aliefukuzwa muda huu,
Basi dada nusura huaga hana swaga za kijinga na mimi, hivyo aliondoka ila ghafla akarudi
"oohh shit hebu naomba hio rimoti yako maana yangu haifanyi kazi sjui kwanini?"
Nilimpa rimoti yangu. kwani Dstv tulizo nazo wote ni aina moja na zinaendana
Basi nilivua zangu nguo huku dada nusura akiichukua rimoti na kuondoka zake. Niliingia bafuni na kuyaoga chap chap ili nielekee masjidi, maana mtoto wa kiume naipenda dini yangu vibaya mno.. Nilimaliza kuoga kisha nikavaa kanzu yangu na kutoka chumbani kwangu. Nikaona ngoja nipitie kwa dada nusura ili niichukue ile rimoti
"ooohh basi"
Nilimkuta dada nusura anavaa hivyo niliondoka na kufunga mlango kabisa. ila yeye hana wasi wasi kabisa na hakutegemea kua nitarudi, kwani humu ndani hua wananifanya kama mtoto mdogo vile.... Yaani mfano upo chumbani una badili nguo afu ghafla mtoto wa mwaka mmoja yule wa tee tee yaani anaeanza kutembea. sasa kaingia chumbani kwako na kuku kuta unabadili nguo. mi sidhani kama utajificha au utamwambia arudi, maana ni hajui kitu hata aone nini bado hajui tu....
Sasa hivyo ndivyo wanavyoniona akina zai na nusura. yaani wananiona kama bado ni mtoto mdogo, hivyo hata nikiingia machumbani mwao hua hawashtuki kuniona wakiwa wanavaaa yaani hata kama nimkute na chupi au taiti hawashtuki kabisa, na sijui ni kwanini au kisa mimi ni shoga nini? maana dada nusura hata nikimkuta ana taiti wala hanifukuzi tena ndio kwanza ananikaribisha tena wala haangaiki hata kutupia kanga kwa juuu... na mimi pia hua sinaga taimu nao kabisa coz kuna siku pia nilikua nacheza kalata na dada nusura. mimi ndio nilienda chumbani kwa nusura kwa ajili ya kucheza kalata. sasa nikamkuta ndio anamalizia kuvaa taiti afu mimi ndio nikaingia
"oooo kumbe unavaa? basi?"
"ulikua wataka nini?"
"aaa nilikua nataka tucheze karata"
"sasa si uje"
"vaa kwanza"
"bwana we lete kadi izo"
Ikawa hivyo tena tukajibwaga kitandani kwake. na kuanza kucheza kalata Na muda si mrefu mara zai nae akatokea huku akiwa kavaa kanga moja na chupi tuu.... nae akaja kucheza karata akiwa anakaa hovyo hovyo tu bila kujua mimi mtoto wa kiume nilikuepo maeneo hayo,
"sasa zai si ukae vizuri?"
"weeee nawe kwani nikikaa hivi inakuusu ninj?"
"basi mgeuzie dada nusura kule ila sio mimi"
"waaaiiiiii we cheza karata bwana"
"ivi mbona hamunioni kama na mimi ni mwanaume nyie?"
"we dogo vunga ebu cheza kadi.. wacha kuwaza vitu ambavyo huviwezi. wewe bado mdogo unajua nini wewe?"
Aliniambia hivyo dada nusura huku tukiendelea kucheza kadi. hivyo kwa hali hio na mimi nikajikuta nawazoea kwa tabia yao ya kunikalia uchi mbele yangu. na hata kule kwangu pia wakinikuta na boxer wala hawashtuki wala na mimi sishtuki coz tumezoeana yaani hata nimkute uchi wala sipepesi macho. na hata nikimuangalia simuangalii kwa tamaa ya ngono. kwaio hio tabia imezoeleka sana humu ndani kwetu... na siku hio tulipokua tunacheza kalata. pia mama alikuja na kutukuta tukicheza karata. huku dada nusura akiwa ana taiti na tishet kwa juuu.. afu dada zai amekatia kanga na chupi tu... nikajua kwa hali walionayo ni lazima wagombezwe. lakini nilishangaa ukimya tu tena kwa sifa nyingi
"mmmmhhh? hiii sasa ndio inafaa. yaani mnatakiwa mpendane mkae kama hivi pamoja mcheze karata... hebu ona sasa hata nikijivunia nina watoto si ndio hivi bwana"
"aaa mamaa toka bwana utanchanganya"
"mmmhh yamekua hayo? haya naenda zangu... ila nyie wadada mpendeni mdogo wenu si mnajua yupo mwenyewe?"
"mamaa? mbona unaongea sana? kwani hatumpendi?"
Aliongea hivyo dada nusura huku tukiwa bize kwenye kucheza karata. Mama aliondoka zake huku sisi hatukua tukimuwazia yeye kwa ayasemayo

Kwaio wewe msomaji usishangae kuona nimemkuta zai au nusura ana chupi au taiti afu sijashtuka kitu. ni kwamba tumeshazoeana yaani hata nikimkuta uchi wala sina taimu nae ni kama vile ninapowakuta au wanaponikuta tunakua na akili za kitoto... lakini hii inachangiwa na malezi mabaya sana ya mama angu
...
Ok sasa tuendeleee

Nilipofungua mlango kwa dada nusura ili nikachukue rimoti, nilimkuta anavaa hivyo sikutaka kuingia. kwahio nilipitiliza zangu mpaka kwenye friza na kuchukua juice na kuitupia tumboni. kisha nikatoka zangu nje na baiskeli kwa ajili ya kuenda masjidi.. ilikua ni kama mida ya saa 12 kasoro hivi jioni...

Sasa ile natoka kwenye geti letu la nje nilishangaa kumuona ticha fau akishuka kwenye gari yake ili aje mpaka nyumbani... Aisee leo nampa makavu laivu. coz hawezi kunikosesha amani kila ninapotembea kwa kumkwepa yeye.
"unaenda wapi?"
Nilimuuliza huku nikiwa nimesimama katikati ya njia kumaanisha kwamba sitaki apite
"kwanini umenikimbia shule"
"ivi ticha? ebu nikuulize swali... kuna jambo lolote la maana ambalo unaweza kuniambia ni kwanini unanifata fata?"
"wewe mwenyewe unajua"
"sasa sikia fau... kuanzia leo sitaki mazoea na wewe na usitake niishi kwa kujificha kisa wewe... kama unataka wanaume si uende kwenye madanguro huko? au ukisex na mimi utapata dhahabu? ebu nitolee ujinga hapa, we ni mwalimu wa aina gani unataka kujidhalilisha kwa watoto?"
Niliongea kwa hasira afu kwa sauti kubwa. mpaka dada nusura alitoka nje.. Sijakaa vizuri mara mama nae ndio anakuja kutoka kazini. alifika pale kisha akauliza
"kuna nini hapa mwanangu?"
"si uyu mwalimu hapa?"
"kafanyaje uyo mwalimu?"
"muulize akuambie mwenyewe"
Mama akamgeukia mwalimu na kumuuliza
"eti mama kuna nini na kijana wangu?"
"mwanao ni mkorofi hafiki shule ni mjeuri. sasa leo nilikua nakuja kwa wazazi wake ili nimshtaki"
Mama akanigeukia mimi
"eti sheby? we hufikagi shule?"
"mama mama huyu mwalimu ni muongo huyu.. kama sifiki shule? mbona zai leo kanipeleka mpaka mlangoni je sifiki shule mimi au tabia yako we mwalimu?"
Mara zai akaja huku akisema.
"heeee sheby? huyu si yule mwalimu uliesema anakufatilia huyu?"
"ndio yeye"
Mama akamfata mwalimu na kumuuliza
"we mschana? unamfatia nini mwanangu"
"mama mwanao kiburi huyo"
"weeeeeee mschana chunga mdomo wako huo nitakuitia police sasa hivi hapa, hebu niambie vizuri unamfatia nini mwanabgu?"
Mimi nikasogea kisha nikamuita mama
"mamaa? ngoja mimi niseme ukweli wake"
"ukweli gani huo?"
"huyu mwalimu kuna siku aliniambia nikaone nyumbani kwake... lakini cha ajabu na cha kushangaza akaanza kunitaka kimapenzi ndio mimi nikamkatalia na kumtoroka... sasa toka siku ile nimtoroke hadi leo bado ananifata fata tuuu"
"heeeeeee we mschana? ivi unajua uchungu wa kuzaa wewe? nakuuluza ivi unaujua uchungu wa kuzaa?"

Ticha alikua kimyaaa... sasa dada zai kama unavyomjua Aaanasuta huyo uuuwiii ni shida
"heeee kwanza haka ni kamwalimu haka? mbona hakana hata shepu ya kutembea na mdogo wangu... au unalingia na hako ka prado kako? sikiliza bibie hio gari tunaweza tukakununulia kama kumi hivi.. kwaii huna hadhi ya kutembea na mdogo wetu... pita ivi kwendraaa zako uko.. kwanza jisura lenyewe limekupalama kama kama sio mwalimu vile.. kwanza hata hufai kua mwalimu, puuuuuuuu hata haya huna? jitu ziiimaa lamfata mtoto duuuu Aaaachukuuchaa utalibeba hilo"
Duuuuuu ticha alisutwa na akasutika yaani alijuta kuja hadi nyumbani na kukifanya anajua kupenda sana.... Yaani amshukuru dada nusura kwa kuja kumstopisha
"we zai kua na adabu kidogo basi"
Mama akadakia juu kwa juu
"mwache asutwe si kihere here chake"

Mwalimu fau alikua anatamani kulia maana hakutegemea kama atakutana na familia kichaa kuliko kawaida... na hapa dada nusura kamstahi tu maana akiamua kusuta heeeee ticha atajiona kama hana nguo kwa kusutwa

Sasa ticha akaona hapa ishakua kirambasi akaanza kuondoka taaratibu huku akianza kunipakazia vibaya
"waaapi mnaona mnae kidume na wakati ni shoga uyoo"
"shoga umemzaa wewe? uyooooo unapondea kisa kakunyimaaaa"
Ni zai ndio alimropokea hivyo huku akimsindikiza na kusuta juuu.....
Ila lile neno la kuambiwa shoga lilimgusa mama angu na kumkosesha raha kabisa, mama angu alikua anataka kulia kwa kusikia hilo neno la shoga. Ticha aliingia kwenye gari kisha akatoka mbio. Sasa mama angu nae akaangua kilio kwa kuchomwa na lile neno la shoga.... Ila kwa mimi halinitetemeshi kwakua mimi najijua mwenyewe ni mzima na sina shida. Daaa niliairisha hata kwenda msikitini hivyo tukaanza kumbembeleza mama huku tukimuingiza ndani, maana si tulikua tukigombaniana nje?

Basi siku hio ilipita na leo ni siku nyingine ya juma mosi mida ya saa 2 hivi asubuhi. nilikua zangu chumbani nikifanya mazoezi ya kupiga pushapu na kuruka ruka huko huko ndani kwangu.. Mara mama kafika
"sheby?"
"naam mamii?"
"unafanyaje uko?"
"amna naweka mwili sawa tu"
"ebu jiandae kuna safari tuende"
"wapi mamiii?"
"we jiandae tu mwanangu"
Mmhh Basi niliingia bafuni na kuyaoga fresh kisha nikatoka huku nikiwa nimeshavaa kikawaida tu. Nilitoka huku dada nusura akiniuliza
"sheby? mnaenda wapi na mamii?"
"mmhh mi sijui, coz kanambia tu nijiandae kuna safari"
"mmhhh haya safari njema"

Mara mama akaniita huku akiwasha gari yake
Nikaenda na kupanda gari kisha tukaondoka zetu
"mamii tunaenda wapi?"
"we tulia tu mbona una maswali mengi hivyo?"
Mmhhhh nilitulia tu huku mikiwa nimeshika ipad yangu ya mziki.. nikiwa nasikiliza nyimbo za kiislamu, Nilishangaa kuona tunaelekea moshi
Sikuuliza bali nilikaa kimya huku nikiendelea kusikiliza kaswida

Ilituchukua kama masaa mawili hivi hadi kufika mosh huko ndani ndani huko machame huko. kuna pori zito kweli. na sijui kwanini tumekuja huku
"tushukie hapa"
Mama aliniambia hivyo huku akizima gari
"mamaa? yaani tumeshuka na mpori wote huu?"
"we unaogopa nini? hebu twende kwa miguu"
"mamiii mi siendi mpaka uniambie tunaenda wapi?"
"sheby?"
"naam"
"mimi ni nani wako?"
"si mama angu"
"kwaio unanisikiliza au unakataa?"
"daaa lakini mama?"
"lakini nini sheby? hebu twende"
"aaaaa sawa ila mi nikiona vp narudi"
Tulitembea kati kati ya msitu huku nikisikia miungurumo ya hapa na pale tena. afu kama kulikua na watu wakipita nyuma kwangu ila sikua nawaona, Tulifika mahali tukaskia muungurumo wa ajabu ambao sikuwahi kuusikia toka nizaliwe. ni muungurumo wa kishetani shetani
"mamaa huko siendi bwana"
Sasa mama angu yeye alikua mbele. mara ghafla nikaona vyungu vikiwa juu juu. huku vingine vikiwa vimezungushwa katika eneo hilo. Nilishindwa kuelewa huku kupoje maana toka mwanzo sikua nikiviona...

Sasa toka saa hio namuita mama angu naona hageuki na wala hanitazami kama nakuja au laaa
"mamaa? mamaa? we mamaaa?"
Niliita lakini hakugeuka wala kuitika hivyo nikawa sihitaji kwenda huko kwa vile ambavyo nimeviona kwa ghafla ghafla tu. Nilijiuliza mama ana nini mbona haitikii? Nilikaza ili nikamguse kwenye bega na nimuulize ni kwanini haniitikii?
Nilijitahidi lakini sikua nikimkuta maana alikua katika mwendo mkali mno
"aaaaa mamaa mi siji tena uko"
Ghafla mama angu akageuka na kuniangalia kwa hasira hizo
Heeeeeee nilishangaa kuona sura ya mama angu imekuaje tena?

Itaendelea.....toMorrow

Je? mama yangu ana sura gani? na je? tunaelekea wapi asipotaka kupasema?

Usikose Keshokutwa



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: