Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameamua na ameitangaza kesho, Alhamisi, Novemba 5, mwaka huu, 2015, kuwa Sikukuu na siku ya mapumziko.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano leo Ikulu imebainisha kuwa Rais Kikwete amefanya uamuzi huo, ili kuwawezesha Watanzania kushiriki katika sherehe za kuhitimisha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne na kuingizwa madarakani Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, Naye Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Yohana Sefue katika taarifa yake amesema Rais Kikwete ametoa uamuzi huo kwa mujibu wa mamlaka aliyo nayo chini ya Kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa.
Rais mteule Dkt John Pombe Magufuli anatarajia kuapishwa kkesho kuwa rais wa Tanzania kwa miaka mingine mitano kufuatia kumshinda mpinzani wake Edward Lowassa katika uchaguzi mkuu uliofanyika oktoba 25 wiki iliyopita.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment